January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tetesi za soka Ulaya

Liverpool na Real Madrid zote zitajaribu kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21, kutoka Paris St-Germain msimu ujao. (L’Equipe – in French)

Journalist reveals whether Spurs expect Dele Alli to leave this transfer  window - Spurs Web - Tottenham Hotspur Football News

Real Madrid haina mpango wa kumsajili kiungo wa England Dele Alli, 24, kutoka Tottenham. (Talksport)

Crystal Palace imekana kutoa ofa ya £25m kwa ajili ya kusamjili mchambuliaji kinda wa Liverpool na timu ya taifa ya vijana ya England chini ya miaka 21 Rhian Brewster, 20. (Goal)

Everton wako kwenye mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Atletico Madrid na Colombia Santiago Arias, 28. (Liverpool Echo)

Mlinzi wa kushoto wa Porto Alex Telles ana matumaini ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United ingawa klabu hizo hazijafikia makubaliano ya ada ya uhamisho kwa ajili ya Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 27. (Guardian)

Kumekuwa na mabadililko ya nia ya Manchester United kumsajili Telles baada ya kufungwa na Crystal Palace, jumamosi. (Manchester Evening News)

Lakini juhudi za kumuuza Diogo Dalot, 21, kwenda Porto kama sehemu ya mpango huo kugomewa na klabu hiyo ya Ureno. (O Jogo – via Mirror)

Mashetani wekundu hao wanania pia ya kumsajili mlinzi wa RB Leipzig na Ufaransa Dayot Upamecano, 21. (Telegraph)

Sevilla imethibitisha kwamba imekataa ofa kwa ajili ya mlinzi wake Jules Kounde. Mfaransa huyo anayecheza timu ya taifa ya chini ya miaka 21 amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Manchester City. (Goal)

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya vijana ya Liverpool Bobby Duncan, 19, anajiandaa kuondoka Fiorentina na kuitumikia Derby County. (The Athletic)

Mshambuliaji wa Kihispania Alvaro Morata, 27, anakaribia kurejea Juventus kutoka Atletico Madrid. (Goal)

Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 33, amekubali kuvunja mkataba wake na Barcelona ili kujiunga na Atletico Madrid. (RMC – via Mail)

Spartak Moscow inamtaka beki wa kulia wa Tottenham na Ivory Coast Serge Aurier, 27. (Sky Sports – via Boot Room)

Torino imepunguza nia yake ya kumsajili kiungo wa Arsenal na Uruguay Lucas Torreira lakini Atletico Madrid iko makini kumnasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mail)

Arsenal itamjumuisha Torreira kwenye mpango wake wa kumpata kiungo wa Atletico na Ghana Thomas Partey, 27. (El Gol – in Spanish)

Fulham wanajaribu kumshawishi kiungo wa Leicester City na Ghana Daniel Amartey, 25. (Football Insider)

Southampton inamtaka kiungo wa Benfica Florentino Luis, 21. (Sun)

Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema itakuwa ngumu kwa klabu hiyo kumbakiza Wilfried Zaha kama ofa kubwa italetwa kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, 27. (Talksport)

Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 33, amepelekwa Real Madrid ili wamsajili baada ya kuondoka Paris St-Germain. (Marca)

Leeds imepeleka ofa ya pili kwa ajili ya mlinzi wa Brighton Haydon Roberts, 18. (Football Insider)