KOCHA wa Chelsea Frank Lampard ameelekeza macho yake kwa kiungo wa kati katika klabu ya West Ham na England Declan Rice, mwenye umri wa miaka 21, kuhakikisha anainasa saini yake (Times – subscription required).
KLABU ya Manchester City na Manchester United zinapigana vikumbo kuwania saini ya beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly mwenye umri wa miaka 29, na beki wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 25 Milan Skriniar raia wa Sloviakia. (Independent).
Klabu ya Chelsea na Real Madrid zote zipo mbioni kupata saini ya kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic – Savic mwenye umri wa miaka 25 raia wa Serbia. (Gazzetta dello Sport, via Express).
Klabu ya Crystal Palace imetenga dau la pauni milioni 25 kumnunua mshambuliaji wa Celtic na timu ya Taifa ya Ufaransa Odsonne Edouard, mwenye umri wa miaka 22. (Sun).
Bayern Munich inatarajia kumpiga chini beki wake David Alaba mwenye umri wa miaka 28 raia wa Austria, ambaye kandarasi yake inakamilika 2021. (Mirror).
Klabu ya RB Leipzig inayoshiriki Ligi Kuu Ujerumani, inatarajia kumuongeza mkataba beki wake Dayot Upamecano, mwenye umri wa miaka 21 raia wa Ufaransa ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika 2021, huku akihusishwa kutaka kutimkia Arsenal. (Mirror).
Juventus ipo mbioni kumsaini kiungo wa kati wa Chelsea na timu ya Taifa ya Italy Jorginho, mwenye umri wa miaka 28 mwishoni mwa msimu huu. (Tuttosport, via Sun).
Real Madrid haina mpango wa kumsajili mchezaji yeyote mwisho wa msimu huu kutokana na athari za mlipuko wa corona. Badala yake , klabu hiyo inatumai itachangisha pauni milioni 190 kupitia uuzaji wa wachezaji huku winga wke Gareth Bale, 30, akihusishwa na uhamisho. (Marca, via Star).
Kocha msaidizi wa klabu ya Aston Villa Dean Smith, anatarajiwa kuwa mkufunzi mpya wa klabu ya Bristol City. (Football Insider).
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM