December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tetesi za soka Barani Ulaya leo Julai 14, 2020

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

RAIS wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu, amekataa kuwa mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar,28, kurejea tena Camp Nou huku wakifikiria uhamisho wa mshambuliajji wa Inter Milan raia wa Ajentina Laitaro Martinez, mwenye umri wa miaka 22. (TV3 Mundo Deportivo).

Bartomeu pia amesema ana ”uhakika” mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi(33), atasalia katika klabu hiyo zaidi ya mwaka ujao. (TV3 via Evening Standard).

Manchester City itatoa ofa kwa kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola mkataba wa muda mrefu baada ya kushinda rufaa yao. (Mirror).

Guardiola atapatiwa karibu kitita cha pauni milioni 150 kwa ajili ya kukipa nguvu kikosi cha Man City. (Guradian).

Real Madrid inaamini kuwa mshambuliaji Kylian Mbappe ,21, atakuwa na mazungumzo nao kuhusu uhamisho kutoka Paris St-Germain. (Marca).

Liverpool ina mpango wa kumuuza beki wake Dejan Lovren, mwenye umri wa miaka 31, licha ya kutaka kuongeza mkataba wake. (Goal).

Bayern Munich wapo kwenye mchakato wa kunasa saini ya Tanguy Ndombele, mwenye umri wa miaka 23, anayekipiga katika klabu ya Tottenham pamoja Mfaransa mwenzie anayecheza nafasi ya kiungo cha kati kwenye klabu ya Monaco, Tiemoue Bakayoko, mwenye umri wa miaka 25. (Le 10 Sport via Daily Mail).

Nice imetoa ofa kwa kiungo wa kati Muhispania Rony Lopes anayekipiga Sevilla. (RMC Sport-in French).

Brentford inamlenga winga wa Portsmouth Ronan Curtis, mwenye umri wa miaka 24, kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Said Benrahma iwapo ataondoka kwenye klabu hiyo. (The News, Portsmouth)