October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jiji la Mwanza. Picha ya mtandao

Tetemeko latikisa Kanda ya Ziwa

Na Mwandishi Wetu,

TETEMEKO la ardhi limetokea katika Ukanda wa Ziwa Victoria na kuyakumba maeneo ya mikoa ambayo ni jirani na ziwa hilo ikiwemo eneo la mpaka wa Geita na Shinyanga.

Mmoja wa wanajiolojia kutoka taasisi ya Jiolojia akizungumza kwa sharti la jina lake kuchapishwa gazetini alithibitisha kutokea  tetemeko hilo lina ukubwa wa 4.6 katika vipimo vya Richta.

Alisema amesema Tanzania imepitiwa na mkondo wa bonde la ufa la Afrika Mashariki ikiwa na mikondo miwili mkondo wa Mashariki na mkondo wa Magharibi, hivyo matukio ya mateteko ya ardhi kwenye mkondo wa bonde la ufa ni lazima yotokee na kuwataka Watanzania muda wote wawe kwenye hali ya tahadhari.

Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita Mponjoli Lotson amethibitisha kutokea kwa tetemeko katika mkoa wake ambaye akisema tetemeko hilo haijasaabisha madhara.

Mkoani Shinyanga hasa katika wilaya ya Kahama ambayo inapakana na mkoa wa Geita kupitia kwa Mkuu wa  wilaya hiyo, Anna Mringi Macha amethibitisha kutokea kwa tetemeko hilo akisema halijaleta madhara.