Na Esther Macha , Timesmajira Online, Songwe
Wakulima wa zao la Kahawa nchini wameanza kunufaika na matumizi ya teknolojia za kisasa za mashine za kuchakata zao la kahawa kuanzia kilo 300 mpaka 5,000 hadi 20,000 kwa saa moja.
Akizungumza na Timesmajira Majira, Meneja Mkuu wa kampuni ya Jm Estrada kutoka Medellin nchini Colombia ,Sandra Cardenas amesema kuwa teknolojoa hiyo haitumii maji kabisa na imekuwa ikitumika kwa nchi ya Colombia kwa zaidi ya miaka 30.
Cardenas amesema hayo kwenye banda la maonyesho la kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhmisho ya siku ya kahawa duniani yaliyofanyika katika kiwanda cha kukoboa Kahawa Mbozi (MCCO)MKOANI Songwe.
“Tulifika Tanzania miaka 30,iliyopita Mimi na mume wangu yeye alikuwa anafanya kazi ya kuzalisha kahawa aliona ubora wa kahawa wameharibu walikuwa hawatoi sukari na hivyo kuharibu ubora wa kahawa na kupata bei ndogo , kwenye miti ilikuwa nzuri lakini waliharibu wakati wa kufanya utaratibu wa kutoa sukari Mume wangu alijua kule Colombia kuna teknolojoa mpya ambayo ni nzuri ambayo aliamua kuleta Tanzaniari isaidie wakulima wa kahawa “amesema Meneja huyo.
Amesema kuwa baada ya kufika Tanzania waliona kahawa kwenye miti ni nzuri lakini walifikiri kuleta Teknolojia hiyo kwasababu waliona watu hawajua hatua za kutoa sukari na wakitoa maganda ni lazima kutoa sukari kisha kukausha na watu wanapata fedha kidogo kwenye kahawa yao.
“Hapa Mbozi wakulima wanapata bei nzuri na wakulima wamebadilisha maisha yao kutokana na mashine hiyo mpaka Sasa ni miaka 25 hivyo Teknolojia hii ni msaada mkubwa Sana kwa wakulima mikoa mingine ambao hatujawafikia tuwasiliane kwa namba ,0784318242 “amesema .
Aidha Meneja Cardenas amesema kuwa awali walileta teknolojoa hiyo kwa kampuni moja iliyopo Tanzani ambapo waliuza sana ambapo walisaidia sana wakulima wa Mbinga, Kilimanjaro,Mbozi na miaka 15 iliyopita waliboresha na kwenda Colombia kutafuta nzuri zaidi kwani iliyokuwa ilikuwa ina tatizo kidogo na iliyopo sasa inatoa kutu na kitu unisaidie inaingia kwenye kahawa hivyo walibadilisha na mashine hiyo inaitwa Jm Estrada ambayo inalinda vizuri na kutoa kahawa yenye ubora.
“Hakuna hata siku moja mashine inapata kutu kwasababu mashine ina ubora na inalinda ubora wa kahawa hivyo kumfanya mkulima kuwa na kahawa yenye ubora ,maganda ya kahawa wanatoa kwa wakulima wanaangalia eneo lake na kujenga vivuko ili watu wasipate ajali”amesema Cardenas.
Hata hivyo Meneja huyo amesema kuwa Teknolojia hiyo inasaidia kwa Tanzania kwasababu hakuna maji mengi pia kutochafua mazingira Sababu hakuna maji machafu nakuwa pia wanaomba maeneo ya kuwatengenezea wateja wao ambao ni wakulima maeneo safi ya kukaushia Kahawa na.mwisho utaratibu huo badae inakuwa mbolea hivyo kunakuwa hakuna kuharibu mazingira tena.
Aidha Meneja huyo ameshauri wakulima katika kutumia mashine hiyo ni vema kutumia umene kuliko mafuta kutokana na gharama kubwa ya mafuta kwasababu bei inapungua kila mwezi na kuwa kampuni hiyo ipo Mbozi na Arusha.
Pia Meneja huyo amesema kampuni hiyo ya Jm Estrada wamekuwa wakusaidia vyama vya ushirika na wakulima wadogo kupata mikopo katika kununua mashine ,
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Jm Estrada,Ulf Kusserow amesema kuwa ni wakati Sasa kwa wakulima wa kahawa kuwa na kahawa yenye ubora itamfanya mkulima kuboresha uchumi wake kutokana na ujio mpya wa Teknolojia hiyo.
Kaimu Mkurugenzi mkuu bodi ya kahawa Tanzania,Moses Simwinga amesema kuwa kanda ya nyanda za juu kusini ni eneo ambalo linategemewa kwa uzalishaji wa kahawa aina ya Arabica na kuwa kuna eneo kubwa ambalo lilalimika.
Mmoja wa wakulima wa kahawa Mkoani Songwe ,Atu Simbeye amesema kuwa ujio wa Teknolojia hiyo mpya kwa wakulima itakuwa msaada mkubwa na tayari kwa mkoa wa Songwe tayari wakulima walio wengi wameanza kuona matunda ya msshine hizo.
More Stories
Maofisa Watendaji watakiwa kufanya kazi kwa weledi
Muhoji Sekondari kumaliza changamoto ya umbali kwa wanafunzi Musoma vijijini
Tanzania mwenyeji mkutano wa nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika