January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TDMA kuadhimisha siku ya Ma-Dj Duniani

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online.

CHAMA cha Muziki wa Disco Tanzania (TDMA), Madj nchini wanatarajia kuadhimishai Siku Madj Duniani ambayo yatafanyika kwa mara ya nne.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo, maadhimisho hayo kwa hapa nchini yatafanyika Jumapili kuanzia saa 10 jioni mpaka asubuhi yatafanyika ukumbi wa Club71 Tegeta jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa katika tamasha hilo TMDA, inatarajia kutoa tuzo kwa Ma Djs mahiri wa zamani na wa sasa ambao wametoa mchango mkubwa katika tasnia ya Udj hapa nchini.

Pia TDMA imekusudia kuwasaidia Madj wa sasa kuwa na mwamko mzuri katika maisha na kutumia fursa mabalimbali kujiendeleza.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa tamasha hilo, pia litaambatana na kutambua michango mbalimbali na mafanikio ya Madj’s katika kukuza tasnia hiyo muhimu.

Tamasha hilo limelenga kuwafikia wadau mbalimabali wa tasnia hiyo na hasa kuhamasisha kizazi cha sasa kuwa na maadili mema ya taifa na kulinda heshima ya sanaa hiyo.
Maadhimisho hayo yataambatana na burudani na shuhuda mbalimbali kutoka kwa Madj, waliofanikiwa na kudumu kwa muda mrefu huku wakipambana na changamoto mbalimbali.

Maadhimisho ya mwaka huu, yameandaliwa lengo likiwa ni kuwakutanisha Madj wote, kuungana kwa pamoja na kuweza kuwasaidia kwa hisani, wanajamii wenye kuhitaji mahitaji maalumu na kupambana na kuhamasisha jamii kuepukana na kutumia dawa za kulevya.