November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Profesa Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo kufunguliwa awamu ya pili ya udahili wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2020/2021 (Picha na Mwandishi wetu)

TCU yafungua dirisha la Udahili kwa awamu ya pili mwaka wa masomo 2020/2021

Na Irene Clemence ,TimesMajira,Online 
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inatarajia kufungua rasmi   dirisha la  awamu ya pili ya udahili  wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2020/2021 Novemba 12 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo na Katibu Mtendaji TCU , Prof.Charles Kihampa amesema  awamu hiyo ya pili ya udahili wa shahada ya kwanza itaanza rasmi Novemba 12,2020 na kukamika novemba 18 mwaka huu.
Amesema  kufunguliwa kwa awamu hiyo ya pili ni fursa kwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi  ya udahili au kudahiliwa katika awamu ya kwanza kutokana na sababu mbalimbali hii ndo nafasi yao.
“Tunasisitiza kwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au kudahiliwa kuitumia fursa hii kutuma maombi yao ya udahili katika vyuo wanavyopenda”amesema Prof.Kihampa.
Prof.Kihampa amesema Taasisi za Elimu ya juu zinapaswa kutagaza programu ambazo bado zina nafasi ili waombaji waweze kutuma maombi.
Amesisitiza kuwa waombaji pamoja na vyuo wanahimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa awamu ya pili kama ilivyooneshwa katika kalenda ya udahili iliyotolewa na TCU.
Aidha amewataka waombaji udahili wa shahada ya kwanza kuzingatia kuwa Masuala yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja katika Vyuo husika.
“Kwa wale ambao watapata chagamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa”amesemaProf.Kihampa.
Akizungumza waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja Prof.Kihampa amesema wanapaswa Kudhibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia Sasa hadi Oktoba 17 mwaka huu.
“Waombaji waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja kuanzia leo watapokea ujumbe mfupi wenye namba maalumu ya siri uliotumwa kupitia namba zao za simu au barua pepe ..hivyo waonapo namba hizo za siri ni vema Kudhibitisha udahili wao katika chuo kimoja wapo kwa vile walivyoomba”amesema Prof.Kihampa
Pia amesema awamu ya kwanza ya udahili kwa ngazi ya shahada katika Taasisi za Elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2020/2021  umekamilika ambapo majina yanatarajia kutagazwa na vyuo husika.
Prof.Kahampa amesema katika awamu hiyo jumla ya waombaji 90,572 walituma maombi ya kujiunga katika vyuo 74 vilivyopo katika kuwadahili.
” Jumla ya programu 686 zimeruhusiwa kudahiliwa ukiliganishwa na programu 645 mwaka 2019/2020 huku kwa upande wa nafasi mwaka huu kuna jumla ya nafasi 157,770 ikiliganishwa na nafasi 149,809 mwaka uliopita hii ni ongezeko la nafasi 7,961 za shahada ya kwanza sawa na asilimia 5.3