Na Mwandishi Wetu, TimesMajir Online, Dar es Salaam
KATIKA Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mteja Duniani Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA)imeanzisha mpango maalumu wa kutatua changamoto za huduma za mawasiliano nchini, kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo.
wadau waliowakutanisha ni watumiaji na watoa huduma za mawasiliano Kama kampuni za simu,Ving’amuzi na watoa huduma wa redio na luninga.
Akizungumza Dar es Salaam Jana, katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta Mawasiliano,Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji TCRA, John Daffa,alisema wadau waliowakutanisha ni watumiaji na watoa huduma za mawasiliano Kama kampuni za simu,Ving’amuzi na watoa huduma wa redio na luninga.
Alisema tangu kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo hawajawahi kuwakutanisha watendaji hao na wananchi kwa ajili ya kujadili, kutatua na kusikiliza changamoto za huduma za mawasiliano ana kwa ana.
Daffa alisema kuwakutanisha wadau hao ni sehemu ya Maadhimisho ya siku ya haki ya haki ya mteja ambayo huadhimihwa kila ifikapo Machi 15, na mwaka huu Kauli mbiu ni usawa wa huduma za fedha kigitali.
“TCRA itaendelea kuratibu mikutano ya namna hiyo ili kuweza na pokea na kutatua changamoto za watumiaji na watoaji wa huduma za mawasiliano nchini,”Alisema.
Kwa upande wake Meneja wa kitengo kinachoshughulikia Wateja kutoka TCRA Thadayo Ringo,aliwataka wananchi kuendelea kufanya uhakiki wa matoleo mapya ya simu wanazotumia pamoja na ‘application’ wanazozipakua ili kuepuka changamoto ya matumizi ya bando kuisha kwa haraka.
Ringo alisema TCRA inaendelea kuelimisha jamii kuhusu wizi wa mtandaoni na aliwataka wananchi kujiadhari na njia za mkato ikiwemo kudanganywa katika mashindano mbalimbali kwa kuambiwa umeshinda kiasi fulani cha fedha akiwa haujashiriki.
” Tujiadhari na njia za mkato hizo ndiyo zinasababisha watu wanatapeliwa, kwa mfano mtu unaambiwa umeingia katika shindano fulani ambalo ujawahi kushiriki au kucheza tuwe makini”à lisema
Aidha baadhi ya wadau wa mawasiliano walioshiriki katika mkutano huo wameiomba serikali kuondoa tozo ambazo zimekuwa zikileta vikwanzo katika utaoji huduma.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best