Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
Kampuni ya Sigara (TCC),imeibuka mshindi wa kwanza,katika tuzo za Rais kwa Mzalishaji Bora wa Mwaka Viwa,ambazo zinaratibiwa na Shirikisho la Wenye Viwanda(CTI),ikifuatiwa na kampuni ya bidhaa za plastiki ya Plasco Limited na kampuni ya mabati ya ALAF Limited.
Akizungumza Leo jijini Dar-es-Salaam katika hafla ya utoajia tuzo hizo Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ameipongeza CTI,kwa kuratibu vyema tuzo za wenye viwanda tangu kuanzishwa kwake.
Dkt Mpango amesema tuzo hizo zimekuwa chachu ya maendeleo ya viwanda ambavyo vimekuwa nguzo ya ukuaji wa uchumi kutokana na kuzalisha ajira nyingi.
Amesema sekta ya viwanda ni chimbuko la maendeleo ya nchi na ina fursa ya kukua haraka na kutengeneza ajira,pamoja na kuchochea bunifu na maendeleo ya teknolojia.
Pia amesema sekta ya viwanda ni eneo muhimu la kuongeza ajira nchini na fedha za kigeni.Vilevile ina mchango kwenye ukuaji wa sekta zingine kutokana na kuzalisha bidhaa zinazouzwa nje na ndani ya nchi.
“Licha ya umuhimu wa sekta ya viwanda,kwenye ukuaji wa pato la taifa, mchango wa sekta hiyo hapa nchini bado ni mdogo, wenye viwanda wanapaswa kupambana kukuza sekta hiyo,”amesema na kuongeza;
“Nakumbuka mwaka 2021 niliwapa changamoto,na leo hii narudia tena kuwataka muongeze mchango wenu katika mapato ya fedha za kigeni kwenye uchumi wetu na kwenye ajira rasmi,”amesema.
Hata hivyo amesema moja ya changamoto ya ukuaji wa viwanda ni kushindwa kupata mikopo ya gharama nafuu, uhaba wa rasilimali watu wenye ujuzi, matumizi ya teknolojia yaliyopitwa na wakati, miundombhinu hafifu na vikwazo visivyo vya kodi.
“Katika kukabiliana na changamoto hizi kunahitajika jitihada za pamoja za wadau, kuongeza tija na ushindani kwenye sekta ya viwanda, mzalishe bidhaa ambazo ni nyingi na ambazo zitashindana kwenye masoko ya nje,” amesema Dkt. Mpango.
“Serikali inaendelea kufanya jitihada kuimarisha sekta ya uchukuzi ikiwa ni pamoja na kuimarisha usafiri wa anga,reli, ndiyo maana leo nimelala Dodoma na muda huu niko hapa Dar es Salaam,” .
Hivyo katika jitihada za kukuza maendeleo ya viwanda serikali inaendelea kusimamia ukamilishaji wa ujenzi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere (JNHPP),mpaka sasa ujenzi wake umeshafikia asilimia 99 na mitambo imeshawashwa na kuzalisha umeme.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, alipongeza Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI) kwa namna ambavyo imekuwa ikisimamia utoaji wa tuzo hizo tangu kaunzishwa kwake.
Rais wa CTI, Paul Makanza aliipongeza serikali kwa namna ambavyo imekuwa ikiendelea kuwawekea mazingira mazuri wawekezaji na kusikiliza kero zao.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba