Na Mwandishi Wetu,Timesmajira
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) imetumia Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani(ICAD) kushiriki katika mbio za Marathon zilizoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mbio hizo zilizoongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, zilihudhuriwa pia na Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete .
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) ambayo kilele chake ni Desemba 7,2024. Maadhimisho ya mwaka huu pia inatimia miaka 80 tangu siku hii ilipoanza kuadhimishwa mnamo Desemba 7 mwaka 1944.
Watumishi wa TCAA licha ya kufanya kazi zao za ki udhibiti na kuongoza ndege pia hushiriki katika michezo mbalimbali ikiwa ni hatua ya kuweka afya katika hali bora wakati wote.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
Samia awazawadi Stars milioni 700/-