January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TCAA kutoa motisha kwa vijana wanaofanya vizuri masomo ya usafiri wa anga

Na Penina Malundo, timesmajira

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga nchini TCAA imesema itaendelea kutoa motisha kwa vijana wanaofanya vizuri katika masomo ya sayansi hususani katika upande wa uhandisi wa utengenezaji ndege na warusha ndege,lengo ikiwa ni kuongeza wataalam wengi katika fani hiyo.

Hayo ameyasema jana jijini Dar es Salaam,Katika kongamano la wahitimu la 10 la Chuo cha Usafirishaji NIT ,Kaimu Mkurugenzi Mdhibiti Uchumi wa TCAA,Rodney Chubwa kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TCAA,Hamza Johari wakati akitoa tuzo kwa mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo ya usafiri wa anga kwa upande wa uhandisi wa Matengenezo ya Ndege katika Chuo cha Usafiri (NIT) kwa kumpa hundi ya kiasi cha Sh. Milioni Moja pamoja na kumpa nafasi ya kwenda kujifunza kwa vitendo katika ofisi zao kwa muda wa mwaka mmoja.

Chubwa amesema mamlaka yao inautaratibu wa kutoa tuzo kama hizo kwa lengo la kutoa hamasa kwa vijana kupenda kusoma masomo ya uhandisi wa ndege na usafiri wa anga kutokana na sekta hiyo kuwa na gepu kubwa la wataalam.

Amesema tuzo hizo zinatoa motisha kwa vijana mwenyewe na wengine wanaokuja kupenda kusoma masomo ya sayansi ili wafanye vizuri katika nafasi hizo na kuja kuziba gepu la Wataalam wa usafiri wa anga nchini.

Amesema wamekuwa na programu kama hizo za kutoa motisha kwa vijana wanaofanya vizuri ambapo tayari wanamfuko maalum wa kusaidia wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi katika maeneo ya uendeshaji wa ndege na uhandisi wa Matengenezo ya Ndege.

”Mipango ipo mamlaka inafanya ikishirikisha wadau katika kuhakikisha gepu la wataalam katika usafiri huu linapungua kwani hatuwezi kulimaliza kwa mara moja,”amesema na kuongeza

”Tunaendelea kuhimiza vijana kupenda masomo ya sayansi na kuyasoma kwani sio magumu kama watu wengune wanavyosema,wanapaswa kukazana na kusoma vizuri kufaulu ili kukava gepu lililowazi la kupata wataalam wengi ambao tutawazalisha wenyewe,”amesema.

Kwa Upande wake Mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Uhandisi wa Matengenezo ya Ndege wa Chuo cha NIT ambaye pia amepokea zawadi ya TCAA baada ya kufanya vizuri masomo yake, Aloysius Rwezaula ameshukuru TCAA kwa kumpa zawadi hizo na kuona ni namna gani juhudi ya kusoma inatambulika na mashirika mbalimbali ni kitu kinachofurahisha.

”Nawaasa vijana wenzangu kusoma kwa bidii ili tuweze kucover gepu la wataalam na zawadi kama hizi waone kama motisha katika masomo yao ili kuweza kuongeza wataalam wengi wa masuala ya usafiri wa anga,”amesema