Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS)limesema lina jumla ya maabara 12 na zote zimeweza kupata ithibati za umahiri,ambapo maabara hizo zimehakikiwa na kupatiwa vyeti vya ithibati ya umahiri wa kimataifa.
Ambapo limesema hatua hiyo inamaanisha kuwa majibu ya sampuli kutoka katika maabara hizo yanaaminika kokote duniani na hivyo kurahisisha biashara ndani na nje ya mipaka ya nchi.
Hayo yamesemwa jijini hapa leo,Machi 18,2025 Mkurugenzi Mkuu wa TBS,Dkt. Ashura Katunzi,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa shirika hilo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Dkt.Katunzi amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita TBS imeweza kupima sampuli zaidi ya ya 118,059 na kufanyia ugezi vifaa 36,808 ambapo suala hilo litasaidia kuhakikisha katika soko kunakuwa na bidhaa zenye ubora.
“Maabara za TBS zina mashine za kisasa (state-of -art-equipment) zinazopelekea kupata majibu kwa wakati na sahihi, pamoja na mashine nyingi zilizopo katika maabara hizo,kuna mashine za kipekee,”amesema.
Aidha Dkt.Katunzi amesema kuwa
Shirika hilo linatumia mifumo ya TEHAMA katika utoaji wa huduma zake mbalimbali kama vile leseni ya ubora, ukaguzi wa shehena zinazotoka nje ya nchi na usajili wa bidhaa za chakula na vipodozi, majengo, maeneo ya uzalishaji, uuzaji, vyombo vya usambazaji wa bidhaa za chakula na vipodozi.
“Mifumo hiyo ni OAS na i-SQMT.Aidha, Shirika limeboresha huduma zake kwa wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa nchini kwa kuunganisha mfumo wake unaoitwa Online Application System na mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Tanzania electronic Single Window System – TeSWS) ambapo mfanyabiashara anatuma maombi na anapata huduma za taasisi zote na kibali kupitia mfumo huo,”amesema Dkt.Katunzi.
Vilevile Dkt.Katunzi amesema
TBS inatambua na kusifu juhudi za Serikali katika kuboresha upatikanaji wa nishati safi, kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, na kutunza mazingira huku ikiokoa maisha kupitia suluhisho endelevu la upatikanaji wa nishati safi ya kupikia.
“TBS ina jukumu muhimu kama taasisi ya viwango nchini katika kuhakikisha utekelezaji wa viwango vya kitaifa vya nishati unasaidia kufanikisha malengo hayo.TBS inashirikiana na washirika wa maendeleo na Wizara ya Nishati kuandaa viwango vya ufanisi wa nishati kwa vifaa vya umeme vya majumbani,”amesema.
Pamoja na hayo amesema kuwa TBS imekuwa taasisi ya kwanza katika Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kupata ithibati (accreditation) ya mifumo ya udhibiti ubora wa bidhaa (Product Certification) ya kimataifa katika wigo mpana (wide scope) ndani ya muda mfupi na ni ya taasisi ya tatu kupata ithibati hiyo iliyotolewa na SADCAS Septemba, 2024 hivyo kufanya mifumo hiyo kutambulika kimataifa.
Pia kwa mwaka 2025, TBS imefanikiwa kupata ithibati ya umahiri wa mfumo wa usimamizi wa chakula katika kiwango cha kimataifa toleo jipya (ISO 22003:2022).
“Kuhamia kwenye ithibati hii kunaifanya TBS kuwa taasisi ya kwanza katika Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kupiga hatua hiyo.
“Ithibati hii ni ishara kuwa TBS inafanya kazi zake kwa kuzingatia miongozo ya kimataifa iliyowekwa na hivyo kuendelea kuaminiwa na wateja na wadau wengine TBS pia tunajivinua kuwa na wataalam wenye umahiri na weledi mpaka kutambulika kimataifa, kwani wataalam wa TBS hualikwa na SADCAS kwa ajili ya kutoa msaada wa kitaalam katika masuala ya ithibati (accreditation) kwenye maeneo ya Metrolojia (metrology), uthibitishaji wa ubora (certification), na ukaguzi (inspection) kwa taasisi na mashirika yanayohitaji huduma hizo katika Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).



More Stories
Puma Energy yawataka wakazi wa Dodoma kuchagua nishati safi
NIT yatumia maadhimisho ya VETA kunadi kazi zao
Wasira atoa siku 14 mnunuzi wa kahawa kulipa zaidi ya milioni 600 za wakulima