Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya
MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA) Msanifu Majengo Daud Kandoro amesema unatekeleza ujenzi wa nyumba 3,500 huku ujenzi wa nyumba 150 ukiwa unaendelea jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu huyo ameyasema hayo alipotembelea banda la TBA katika maonyesho ya Wakulima Nane Nane katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya yanakofanyika Kitaifa.
Amesema lengo la ujenzi huo ni kuhakikisha watumishgi wa umma wanapata makazi bora yatakayowafanya waongeze tija katika kutoa huduma kwa wananchi.
Vile vile Kandoro amesema,pia wanatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya afya katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini .
“Kwa ujumla Nchini kuna miradi tunatekeleza katika mikoa minane ikiwemo ya ujenzi wa vihenge katika utunzaji wa nafaka,pia tuna miradi ya Afya katika wilaya ya Tunduma,Kyela kupitia mradi wetu wa Buni Jenga.”amesema Kandoro
Katika hatua nyingine amesema,pamoja na kujenga lakini TBA pia ni wabunifu wa majengo huku akisema,ujenzi wa awamu ya pili ya mji wa Serikali mkoani Dodoma ubunifu Aidha amesema,hivi sasa wanasimamia miradi 15 ya majengo na wanajenga Ofisi Rais Utumishi katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu huyo amesema,katika kuhakikisha kazi zao zinakuwa na ubora,wanatumia vifaa na mitambo ya kisasa kama vile mitambo ya kuchakata zege uchimbaji na vifaa vingine vinavyotumika katika ujenzi.
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari