Na Joyce Kasiki,Timesmajira online
CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM) kinatarajia kufungua kampasi mpya katika Mkoa wa Njombe itakayoanza kutoa mafunzo mwaka wa masomo 2026/2027 kwa lengo la kupanua wigo na kusogeza kwa wananchi huduma inayotolewa na chuo hicho.
Hayo yamesemwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Wineaster Anderson wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Amesema, ujenzi wa kampasi hiyo utatekelezwa kupitia fedha za mradi wa Hits ambapo kupitia mradi huo chuo kimepokea Dola za Marekani milioni 23 ambapo zinatumika kujenga miundombinu ya madarasa, maabara na kufungua kampasi hiyo mpya katika Mkoa wa Njombe.
Profesa Anderson amesema Kampasi hiyo ya Njombe itajikita kutoa mafunzo katika eneo la misitu, madini, uvuvi na kuziboresha zaidi sekta zilizoko katika mkoa huo.
Akizungumza kuhusu uwepo wao katika maonesho hayo amesema,wamekuja na bidhaa za kipekee zilizobuniwa na wanafunzi wanaosoma katika chuo Kikuu cha Dodoma.
“Chuo chetu kinafanya ubunifu kupitia tafiti mbalimbali zinazofanywa na watafiti wetu na baada hapo hubuni bidhaa kulingana na tafiti husika ambayo inakwenda kutatua changamoto katika jamii ,hii ninkwa sababu tafitinzetu zimejikita katika jamii.”amesema Prof.Anderson
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato