Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye (Mb) jana tarehe 09.02.2022 ,amezindua rasmi Mkutano wa 17 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali mkoani Tanga.
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ni miongoni mwa Taasisi zilizoshiriki kwenye mkutano huo na imetumia fursa hiyo kuendelea kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana kwenye Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Waziri Nape ametumia fursa hiyo kumpongeza Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za dhati za kufungua sekta ya Utalii nchini. Vilevile amewataka Maafisa Habari na Mawasiliano kuhakikisha tovuti na mitandao ya kijamii ya Taasisi inatumia fursa hiyo kutangaza vivutio vya utalii na habari nyingine za Taasisi zinazoisemea.
Naye, Kaimu Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mahusiano kwa Umma- TAWA ,Twaha Twaibu amesema TAWA inashiriki kwenye mkutano huu kwa lengo kubwa la kuendelea kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana kwenye maeneo yao kama jitihada za kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan wa kutangaza vivutio nchini kwa kupitia filamu maalumu ya “Royal Tour” iliyozinduliwa hivi karibuni.
Vilevile, akizungumzia kauli ya Waziri Nape ya kutoa siku 14 kwa Maafisa Habari kutumia tovuti na mitandao ya Kijamii, amesema TAWA imepokea maelekezo hayo na itaendelea kutumia mitandao ya kijamii na tovuti za Taasisi kama nyenzo muhimu ya kujitangaza.
Mkutano huo mkubwa umeshirikisha wadau wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutoka Taasisi mbalimbali za serikali zilizopo Tanzania Bara na Visiwani.h
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi