December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TAWA yatoa elimu ya wanyamapori wakali,waharibifu

Na Mwandishi wetu

JAMII imeshauriwa kuachana na tabia ya kujenga makazi yao karibu na maeneo ya hifadhi za mbuga za wanyamapori ili kujiepusha na hatari zitakazo tokana na wanyama wakali na waharibifu kama Tembo,Nyati,Mambana Kiboko.

Hayo yamebainishwa na Mhifadhi Mkuu anaesimamia Dawati la Ujirani Mwema kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) PC Twaha Twaibu wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari Kwa nyakato tofauti Jijini Dar es salaam juu athari za kufanya shughuli za kibinadamu karibu na hifadhi za wanyamapori

Twaibu amesema jamii inapaswa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa wanyamapori hao kwaajili ya kuepukana na madhara yatakayotokana na Wanyamapori hao

Aidha amewaomba wananchi kutumia fursa hiyo kwa kutoa taarifa kwa haraka pindi Wanyamapori hao watakapoingia katika makazi na kucha tabia ya kupiga nao picha kwani kitendo hicho kinahatarisha maisha yao

Katika hatua nyingine Mkuu huyo amempongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara katika masuala ya uhifadhi,Kwani Kwa kipindi alipokuwa Makamu wa Rais ndiye aliyezindua Jeshi la Uhifadhi.

Kwa upande weke Afisa wanyamapori kutoka TAWA Joseph Mnyai amesema kuwa kunafaida nyingi zinazopatikana kupitia uwindaji wa kitalii pamoja na utalii wa picha.

Amesema fedha zinazopatikana uwenda kuchangia shughuli za kimaendeleo kwa wananchi wanaishi kando kando na Mapori ya Akiba,Mapori Tengefu na Maeneo ya Ardhioevu