November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TAWA yashiriki katika mkutano wa uwekezaji nchini Saudi Arabia

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula. Wajumbe wengine ni pamoja na mwakilishi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) Said Habibu Bilibili ambaye ni Afisa anayesimamia dawati la Uwekezaji.

Ujumbe wa Tanzania tarehe 10/3/2022 umekutana na Shirikisho la wafanya biashara wa Saudi Arabia kuelezea fursa za uwekezeji nchini Tanzania na wameahidi kuja Tanzania kupata maeneo ya uwekezaji ikiwemo kuhudhuria maonesho ya biashara (Sabasaba) mwaka huu ili kuona fursa za uwekezaji.

Aidha,mkutano huo pia umehudhuriwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Mashimba Ndaki na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe Balozi Ali Jabir Mwadini.

Katika mkutano huo ulifanyika Riyadh nchini Saudi Arabia, Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo la wafanya biashara Bw. Tariq Al Haidary ameshukuru sana ujio wa ujumbe kutoka Tanzania na kuahidi kutumia vema fursa za uwekezaji ziliko Tanzania.