Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar
UBALOZI wa Marekani nchini Tanzania, umesitisha huduma zake kwa siku mbili, kwanzia leo Mei 14 hadi 15, kufuatia kuwepo na tatizo la Intaneti lililotokea Mei 12, likisababishwa na kukatika kwa nyaya za chini ya bahari (Subsea Cable), ambayo imeathiri upatikanaji wa mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Msemaji wa Ubalozi wa Marekani nchini, kupitia ukurasa wao wa kijamii, Kalisha Holmes, amesema miadi yote ya kikonseli mei 14 na 15 inafutwa na kupangiwa muda mwingine.
Aidha amesema, kitengo hicho cha kikonseli kitafunguliwa kwa ajili ya kuchukua visa na huduma za dharura kwa raia wa Kimarekani.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi