Na mwandishi wetu, Timesmajira Online
Kampuni ya uuzaji wa Magari makubwa, Madogo na Trela za Mizigo imezindua mpango maalumu kwa ajili ya sekta ya Usafirishaji wa mizigo mikubwa nchini Tanzania kwa kuzindua Trela za mizigo aina ya TIVA Trela itakayomwezesha Mfanyabiashara wa Mizigo au Mkulima kuwa na uhakika wa safari pale anapopakia mizigo katika Trela hizo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja Mauzo na Masoko wa TATA, Smart Deus amesema kuwa, Lengo la uzinduzi wa mpango huu ni kuwaweka karibu wateja na kampuni ya TATA kuelekea katika msimu huu wa mauzo na Mavuno nchini Tanzania( msimu wa Biashara).
Uzinduzi huu umeambatana na uzinduzi wa Trela ya kubebea mizigo Mikubwa kwa wakati mmoja. Pia tumeandaa mpango maalumu kwa wateja watakao wahi kipindi hiki cha mwanzo kuelekea msimu wa mauzo.
“Mwaka 2021/2024 umekuwa mzuri kibiashara chini ya serikali ya awamu ya sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndani ya kipindi hiki milango ya biashara imefunguka na sisi TATA tuna ahidi kushirikiana na serikali, wadau na wateja wetu katika kuleta bidhaa bora kabisa.
Nae Robert Mwakibibi, amesema Mapinduzi haya ni kwenye Usafiri wa umma Daladala, Gari za shule (School buses) au taasisi binafasi/serikali na Trela za kisasa -TIVA Trailers. Katika kuangalia soko letu tumeweka utaratibu wa malipo cash au mkopo wa ndani AFCL na kushirikiana na taasisi za fedha na bank. Ambapo tuna waakikishia wateja wetu huduma za vipuli na ufundi kwa maana ya After sales solutions.

Nae Robert Mwakibibi amesema haya ndio Mapinduzi ya Daladala – usafiri wa Umma na gari za shule (School buses), TATA tumeona soko linauhitaji mkubwa sana wa usafiri salama kwaajili ya Wanafunzi wa shule na Umma, taasisi za serikali na binafsi. Kupitia sekta ya usafirishaji ina kwenda kuongeza fursa, ajira, ulipaji wa kodi, kuleta chachu ya sekta na kuongeza usalama wa barabarani kwa kutumia vyombo vilivyo bora.
“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunaendelea kuwa wauzaji na watoaji wa huduma bora katika sekta ya usafirishaji ili kuyafikia mahitaji na kuleta chachu kwa sekta ya usafirishaji kwa Watanzania hapa nchini kwa bei nafuu na ubora wa hali ya juu.” Ameongeza Smart Deus
More Stories
Madiwani Ilala walia na dampo la Pugu
TLS yaishauri serikali kuanzisha chombo maalumu
Ridhiwani ataka watu wenye ulemavu wapewe fursa