Na Mwandishi wetu,TimesmajiraOnline
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mohamed Salum amesema sekta ya bahari ndiyo inaongoza kwa mchango mkubwa kiuchumi hasa katika shughuli za usafirishaji.
Salum ameyabainisha hayo alipotembelea katika Banda la Taasisi hiyo lilipo katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea.
Amesema sekta hiyo inazofursa nyingi ambazo wananchi wamekuwa hawazifahamu ikiwemo maeneo ambayo wanaweza kusoma na kupata ajira kwa urahisi zaidi.

Hivyo aliwaomba wananchi kutembelea katika Banda TASAC lililopo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ili waweze kufahamu sekta ya bandari na mchango wake katika uchumi.
“Tunawakaribisha watu waje kutembelea banda letu ili waweze wafahamu na kujua kuna fursa gani katika sekta ya bahari . Nchi yetu ya Tanzania inaupungufu mkubwa wa wataalamu kupitia sekta hii zipo ajira na fursa mbalimbali nyingi.
“Duniani kote kuna upungufu wa mabaharia kwa mujibu wa takwimu za uhitaji mabaharia hawajawahi kutosha kwenye Meli”
Aidha amesema Taasisi hiyo inayo majukumu mbalimbali ikiwemo majukum Udhibiti wa usafiri majini pamoja na kuchagiza sekta usafiri nchini .
“Jukumu kubwa la TASAC ni Udhibiti shughuli za usafirishaji majini kwa kuusajili vyombo vinavyojengwa nchini na kuvikagua kila hatua na kuvipa vyeti vya ubora”amesema Salum
Pia amesema wamekuwa wakifanya ukaguzi wa mara kwa mara wa vyombo pamoja na ukaguzi wa meli za kimataifa zinazokuja nchini.



More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi