November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TARI yatafiti mbegu bora zinazokinzana na magonjwa

Na Joyce Kasiki,Dodoma

TAASISI ya Utafiti wa Kilimo (TARI) imesema  inafanya utafiti wa mbegu zinazokinzana na magonjwa ya mazao kwa lengo la kuwawezesha wakulima kuzalisha kwa tija.

Mkurugenzi Mkuu wa TARI ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ishiriki wa taasisi hiyo kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nane nane Nzuguni jijini Dodoma.

Amesema taasisi hiyo imeshafanya utafiti na kwamba wana  aina mbalimbali za mbegu bora za migomba, mbegu za jamii ya mikunde lakini tuna mbegu za mpunga, mahindi na korosho,ambazo uzalishaji wake una tija zaidi.

“Mbegu hizi mbali na kukinzana na magonjwa,mbegu hizo zinatoa mazao mengi zaidi tofauti na mbegu nyingine,kwa hiyo uzalishaji wake una tija kwa mkulima na Taifa kwa ujumla.”amesema

Dkt.Bwana amesema,Taasisi hiyo pia ina Teknolojia nyingine ya  ya kitalu mkeka ambayo pia  inasaidia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Teknolojia hii  inamwezesha mkulima kupanda mpunga kwa muda mfupi,lakini pia  mkulima anaweza kuandaa mbegu hata nyumbani, inasaidia kukimbizana na mvua ambazo zinakua zinabadilika badilikabadilika” amesema Dkt.Bwana

Aidha amesema Taasisi hiyo imetafiti aina mbalimbali za mbegu zinazokabiliana na wadudu, magonjwa pamoja na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo ukame.

Dkt.Bwana amesema hatua hiyo inalenga kutatua changamoto zinazowakabili wakulima zinazotokana na magonjwa, wadudu na hali ya hewa.