January 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tanzanite Queens waichapa Zaimbabwe 10-1 Cosafa

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

KIKOSI cha timu ya Taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 ‘Tanzanite’ kimefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika kusini baada ya kupata ushindi mnono wa goli 10-1 dhidi ya wapinzani wao Zimbabwe.

Ushindi huo mnono ni mwendelezo wa matokeo bora waliyoyapa katika michuano hiyo baada ya awali kufanikiwa kuwafunga Comoros goli 5-1 lakini pia wakiwafunga goli 6-1 wenyeji wa michuano hiyo Afrika Kusini.

Katika mchezo huo, Tanzania ilipata goli dakika ya kwanza lililofungwa na Protasia Mbuda dakika ya kwanza lakini dakika ya 11 Koku Kipanga alifun ga goli la pili na dakika mbili b aada ye Nahodha Irene Kisisa alifunga goli la pili.

Mchezaji Shehat Mohammed aliifungia timu hiyo magoli mawili dakika ya 18 na 89 ambaye pia aliibuka mchezaji bora wakati Ester Ebeneza akifunga goli dakika ya 32.

Kipindi cha pili, Tanzanite waliendeleza ubabe katika mchezo huo baada ya kuongeza magoli yaliyofungwa na Zwadi Athuman dakika ya 55 huku mshambuliaji Aisha Masaka akiendelea kung’ara baada ya kufunga magoli mawili dakika ya 71 na 82 na magoli mengine tyakifungwa na Rudo Machadu dakika ya 79 na Joyce Lema dakika ya 86.

Baada ya ushindi huo sasa timu hiyo inarudi kujiandaa na mchezo wake wa nusu fainali ambao watawakabili timu ya Taifa ya Zambia.