Na David John,Timesmajira Online
SERIKALI ya Tanzania na Ufaransa zimesaini makubaliano ya ufadhili mradi wa Twende Orlimpic Game wenye thamani ya bilioni 1.6 ambao unatekelezwa kupitia makundi mbalimbali yaliyoomba ufadhili huo.
Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa nchini hapa Balozi Nabil Hajlaoui, amesema kuwa makubaliano hayo ya ufadhili yanakwenda kutekeleza mradi wa Twende Orlimpic Game pamoja na kusaidia makundi mbalimbali ya vijana katika mikoa mbalimbali Tanzania ikiwemo Singida ,Dodoma na mikoa mingine pamoja na Zanzibar.
Balozi Hajlaoui amesema serikali ya Ufaransa itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kwenye maeneo mbalimbali na kama inavyofahamika kuwa nchi hizo zimekuwa na mahusiano mazuri tangu huko nyuma.
“Mradi huu unathamani ya bilioni 1. 6 na utakuwa wa miaka miwili na zaidi unalenga makundi ya vijana kupitia mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani,”amesema.
Naye Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo nchini hapa Balozi Dkt. Pindi Chana,amesema kuwa wameingia makubaliano ya utekelezaji wa mradi huo kwa kipindi cha miaka miwili ambao unazingatia vijana.
Amesema kuwa nchi yetu imetoka kwenye sensa na kuonekana kuwa Watanzania wapo milioni 61 kati yao wengi ni vijana hivyo ni namna gani wanaweza kushirikishwa huku akiwasisitiza vijana wote kuwa michezo ni muhimu sana kwani inaleta afya ,ajira.
“Leo hii mchezaji mmoja kutoka timu moja kwenda timu nyingine anahama kwa fedha nyingi kiaisi kwamba timu inanufaika na mchezaji ananufaika hata familia inanufaika, hivi sasa serikali tunakwenda kuboresha mitaala na kuwa na mitaala maalumu ya masuala ya sanaa na michezo lengo nikuwa na Somo ambalo litaweza kufanyiwa hata mtihani wa taifa,”amesema na kuongeza kuwa
“Tunataka kuona mtu anapata cheti na hapa tunachuo chetu cha Malya kinafanya vizuri sana kwa kutoa wakufunzi wa masomo ya masuala ya michezo kwahiyo tunamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Balozi wa Ufaransa kuwa na mradi huu wa Twende Orlimpic Game,”.
Amefafanua kuwa katika Orlimpic zijazo nchi ya Ufaransa ndio mwenyeji hivyo tupo kwenye mchakato wa twende Orlimpic lakini mradi huo pia unahusu masuala ya jinsia kwa watoto wa kike,vijana na michezo mingi itakuwepo na itashirikisha mikoa mbalimbali kama vile Singinda huku akisisitiza watu kuweka ratiba ya michezo ,mazoezi kuazia ngazi ya familia ,shule na taasisi.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha ugonjwa wa Uviko-19 watu walikuwa na tatizo kubwa la kushindwa kupumua na watu wote walihubiri mazoezi na michezo hivyo vitu vinatakiwa viwe sehemu ya maisha na ratiba ya kila siku.
“Nawapongeza wote walioweka shule zote za Academy kuhusu michezo lakini pia watu wanaendesha ligi mbalimbali kwani kila Mkoa wabunge wameweka michezo hivyo watu washirikiane kwenye michezo na ukifanya michezo unaishi umri mrefu pia,”.
More Stories
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo