May 5, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tanzania,Kenya zasaini makubaliano ya ushirikiano sekta ya Nishati

Ni kupitia mauziano ya umeme na upembuzi yakinifu mradi wa Bomba la Gesi Tanzania- Mombasa

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

Waziri wa Nishati Deogratius Ndejembi na Waziri wa Nishati na Petroli wa Jamhuri ya Kenya,Opiyo Wandayi wamesaini makubaliano ya ushirikiano ya kuanza mauziano ya umeme baina ya Tanzania na Kenya pamoja na upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa.

Makubaliano hayo yamefanyika Mei 04, 2026 Ikulu jijini Dar es Salaam mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kenya, Dkt. William Samoei Ruto ambaye yuko nchini kwa ziara yake ya kitaifa.