November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tanzania yachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Maji

Na Mwandishi wetu

TANZANIA imechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Maji Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (ZAMCOM) katika mwaka 2024-2025 kwenye Mkutano wa 11 wa Baraza hilo unaoendelea mjiji Tete Nchini Msumbiji.

Uchaguzi huo umefanyika kufuatia Msumbiji kumaliza muda wake na kukabidhi uenyekiti kwa Namibia, Hivyo, Tanzania inategemewa kuwa Mwenyekiti wa ZAMCO mwaka 2025/2026.

Katika mkutano huo, Tanzania imewakilishwa na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew.

Licha ya kushiriki Mkutano wa 11 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (Zambezi Watercourse Commission – ZAMCOM), Tanzania imefanya mazungumzo na wadau wa maendeleo na kuwakaribisha kuwekeza katika Sekta ya Maji nchini Tanzania.

Mhandisi Kundo ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo amekutana na kufanya mazungumo na Mwakilishi wa Shirika la Sweden, SwedFund.

Katika mazungumzo hayo, Tanzania imeikaribisha Taasisi ya SwedFund nchini ili kushirikiana katika maeneo ya maandalizi ya miradi ya miundombinu yenye ukubwa wa kati na wa juu.

Nae mwakilishi wa SwedFund ameahidi kushirikiana na Tanzania katika kufanya majadiliano kuhusu kuandaa miradi mahsusi.

MWISHO