January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tanzania yaanza kutekeleza mpango wa kuvutia mitaji kutoka China

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kimeanza kutekeleza mpango maalum wa kuvutia mitaji ya Uwekezaji kutoka China ili kuhakisisha Uwekezaji kutoka China unaongezeka.

Mpango huo ni matokeo ya ziara ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa FOCAC nchini China.

Katika mkutano huo Rais wa Jamhuri ya China Mhe. Xi Jinping aliahidi kiasi cha dola bilioni 10 kuwekezwa Afrika kupitia mpango maalum wa kukuza uwekezaji Afrika.

Kufuatia ahadi hiyo ya Rais wa China kuwekeza mitaji Afrika, Waziri wa Mipango na Uwekezaji Tanzania Mhe. Prof. Kitila Mkumbo aliiagiza TIC kuwa na mkakati wa kuhakikishe angalau theluthi moja ya mitaji hiyo ambayo ni dola bilioni tatu inawekezwa Tanzania kutoka China.

Ni kutokana na dhamira ya utekelezaji agizo hilo TIC imezindua Kituo cha kuvutia uwekezaji nchini China katika Jimbo la Hunan ambalo limeteuliwa kuwa lango la uwekezaji kutoka China ili kuhamasisha na kutangaza fursa za Uwekezaji zilizopo Tanzania na kuleta mitaji ya Uwekezaji Tanzania kutoka China.

Jukwaa hili limezinduliwa na Kaimu konseli Mkuu Mhe Ali Mohamed Mwinyi, anayesimamia Ubalozi mdogo wa Tanzania nchini China uliopo jimbo la zenye lengo la kuwekeza Afrika.

Akiongea katika tukio hilo ambalo lilikutanisha makampuni zaidi ya 150 kutoka sekta mbalimbali nchini China wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC ndg. Gilead Teri amesema jukwaa hilo ni mwanzo wa utekelezaji wa mpango wa kuvuta uwekezaji kutoka China na tunatarajia ongezeko la wawekezaji wengi kutoka China kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Viongozi hao baada ya uzinduzi walipata fursa ya kutembelea viwanda vikubwa nchini China kwa lengo la kuvishawishi kufanya uzalishaji kupitia Tanzania