March 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tanzania One yatoa msaada kwa wanawake hospitali ya Temeke.

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Temeke

Shirika la Tanzania One, limesherekea siku ya Wanawake Duniani kwa kutoa vitu mbalimbali kwa wanawake walijifungua hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, jijini Dar-es-Salaam.

Akizungumza Machi 8,2025,Ofisa Habari wa Tanzania one Animation Dumah,amesema,wametoa sabuni,maji,pampers,ikiwa ni sehemu ya kusaidia jamii.

Amesema shirika hilo limesajiliwa mwaka 2024 na lina wanachama 500 kwa Mkoa wa Dar-es-Salaam.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa shrika hilo Samwel Mholo,amesema Shirika wanashughuli za kijamii,afya na mazingira,huku akiitaka jamii kutenga muda kwa ajili ya kutembelea wagonjwa au watu wa mahitaji maalum na kuwasaidia