Na Penina Malundo,Timesmajira
TANZANIA ni miongoni mwa nchi iliyonufaika na Mto Nile kupitia miradi mbalimbali ya Kimaendeleo ya Kijamii(LAPD)ikiwemo Miradi ya Maji,Zahanati,Maboresho ya Shule za Sekondari pamoja na Ujenzi wa Ofisi ya Wilaya ya Ngara na kufanya wananchi wa maeneo mbalimbali waishio pembezoni mwa mto huo kunufaika.
Miradi hiyo imekuja katika maeneo hayo baada ya utekelezaji wa Mradi Mkubwa wa Kufua Umeme wa maporomoko ya Rusumo uliopo katika Mpango wa Bonde la Mto Nile (Nile Basin Initiative NELSAP)ambao umefadhiliwa na Benki ya Dunia.
Mratibu wa Kikanda wa Mpango Tanzu wa Nile Equatorial Lakes (NELSAP -CU),Mhandisi Dkt. Issac Alukwe anasema miradi hiyo ya LADP uchaguliwa na wananchi wanaoishi pembezoni mwa mradi huo wa umeme wa mto Rusumo ambao utoa vipaumbele vyao vinavyoonesha sehemu gani zinachangamoto na kuweza kuzitatua kwa kusaidiwa kuwezeshwa na NELSAP ikiwemo katika maeneo yao.
Dkt. Alukwe amesema mradi wa rusumo kwa Tanzania umekuwa na manufaa makubwa licha ya kwamba kiasi cha umeme ambacho kinainga kwa Tanzana ni kidogo ukilinganisha na vyanzo vingine vya umeme vilivyopo Tanzania.
”Kiasi cha umeme kinachoingia Tanzania kutoka rusumo ni kidogo ukilinganisha na vyanzo vingine vilivyopo ndani ya nchi hiyo vinavyozalisha umeme,lakini ukiangalia miradi ya Local Area Development iliyowekeza Tanzania imenufaika kikubwa,”amesema.
Akitaja miongoni mwa miradi hiyo ya LADP ambayo wametekeleza ni pamoja na ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Ngara (Ngara Headquater),Soko la Kimkakati eneo la Kaaza Rusumo,Kituo cha Afya cha Rusumo,Uboreshaji wa majengo ya Shule Sekondari ya Ngara pamoja na Mradi wa maji wa Rusumo (Ngara Water Supply) ambayo yamefikishwa katika vijiji mbalimbali katika kuhakikisha wanapata maji safi na salama.

Dkt.Alukwe amesema mradi mkubwa ambao wanajivunia ni mradi wa Umeme wa Rusumo ambao ni mkubwa na umeleta manufaa makubwa kwa nchi tatu Tanzania,Rwanda na Burundi.
Akitolea mfano kwa nchi ya Burundi namna huduma ya umeme inavyopatikana amesema hali yake ya upatikanaji wa umeme ilikuwa ni asilimia 47 pekee ila baada ya kukamilika kwa mradi na kuuongeza umeme kutoka rusumo sasa umefikia asilimia 74 Megawati,hali ambayo imeongeza kasi ya upatikanaji wa umeme kwa nchi ya burundi kwa asilimia 57.
”Ilikuwa ukifika Bujumbura utasikia majenereta yanalia tu kuwasha umeme ila tangu kuanza kuachia umeme kuingia katika miundombinu ya Burundi matumizi ya genereta kwa burundi yamepungua kwa kiasi kikubwa,burundi imenufaika pakubwa zaidi ya Umeme pia imepata miradi ya Zahanati ,Maji,Majengo ya Utawala na sio Burundi tu hata Rwanda napo wamenufaika pakubwa na mradi huu,”amesema.
Alex Bushahu Mkazi wa Kijiji cha Kasulo Kitongoji cha Ngoma amesema eneo la songambele ni miongoni mwa maeneo ambayo yalikuwa na uhaba wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa kipindi cha muda mrefu.
Amesema awali wananchi wake walikuwa wakichota maji katika madimbwi ambayo yalikuwa yakipatikana kwa umbali wa Kilometa Moja na nusu,ambapo maji hayo yalikuwa si safi wala salama ka matumizi ya binadamu.
Soma zaidi
:https://timesmajira.co.tz/mradi-wa-maji-ulivyorudisha-matumaini-mapya-kwa-wananchi-waishio-mpaka-wa-rusumo/
Bushahu amesema kutokana na uhaba huo wa maji watu walilazimika kuchota maji hayo na kuyatumia ambapo yalikuja kuwaletea madhara makubwa watu kuugua Kichocho na kuhara damu.
”Hali ya wanakijiji cha Ngoma ilikuwa ni mbaya sana katika upande wa maji safi na salama,wamama walikuwa wanaamka usiku kwenda kuchota maji ambapo ukutana na vitu mbalimbali wakiwemo wanyama wakali,”amesema na kuongeza
”Bado ukifika huko utakutana na foleni ambayo ni lazima mtu akae ili aweze kusubiri foleni ipungue zamu yake ikifika na yeye achote maji,huku familia inamsubiri huku mwanaume anataka kumuona mama amerudi mapema basi migogoro ya familia ilikuwa ni mingi kuliko sasa,”amesema.
Ameishukuru NELSAP kupitia mpango wake wa Miradi ya Maendeleo ya Kijamii (LADP) kwa hatua kubwa walioichukua ya kuwasaidia wananchi wa kijiji hicho cha Ngoma kwani sasa hivi hali imebadilika wapo vizuri kiafya na hata migogoro ya familia imepungua .
Amesema kutokana na uwepo wa maji ya uhakika kijiji chao sasa kimekuwa miongoni mwa vijiji vyenye maendeleo watu wameanzisha miradi ya bustani katika magati ambayo yapo karibu na mabomba na kufanya maendeleo yakue kwa kasi.
Amesema kijiji hicho kina idadi ya kaya 30 huku idadi ya watumiaji maji katika kaya hizo ni 150 ambapo kila mwezi kila kaya inapaswa kulipia maji hayo 1000 ambapo ukusanywa na kupelekwa,Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ambapo fedha hizo zinakuwa kwaajili ya ukarabati wa bomba endapo litaharibika na matumizi mengine yanapotokea.
”Kwa kweli tunashukuru sana kwa hatua hii ya NELSAP sasa hivi maji yako karibu na watu wanachota maji muda wowote ule wanapoyahitaji haya ni maendeleo makubwa katika kijiji chetu cha Ngoma,”amesema na kuongeza
”Tunaomba NELSAP isiishie hapa iendelee katika vijiji vingine kusaidia huduma hii iweze kupatikana kwa uhakika na watu waweze kupata maendeleo yao kwani ikiwa muda mrefu watu wanatumia kutafuta maji,maendeleo ukosekana.
Kwa upande wake Mtaokeo Mkuthe Msimamizi wa Mradi wa Maji Benako Benguka Kijiji cha Lakalemela Wilayani Ngara amesema wanaishukuru NELSAP kupitia LADP kwa kuwafanyia maboresho makubwa ya bomba ambalo lilikuwa linategemewa na wananchi wengi wa Benako.
Amesema uboreshaji huo wa bomba umeweza kuwasaidia kwa asilimia kubwa kuondokana na adha ya maji ambapo awali walikuwa wanakumbana nayo kutokana na foleni ya usubiriaji wa maji kuwa kubwa.
Kwa kweli tunashukuru sana sana NELSAP kwa kuja kutufanyia maboresho katika bomba letu na kuhakikisha sasa maji yanatoka mengi na ya uhakika tofauti na miaka ya nyuma maji yalikuwa hayatoki kwa wakati kutoka na miundombinu iliyowekwa tangu zamani kutokuwa mizuri na kutoendana na wakati,”amesemaÂ
More Stories
DC Ubungo kuanza kuwasajili ‘bodaboda’
NEC yachagua wajumbe wa kamati kuu,yumo Asas
Waziri Aweso atoa maelekezo kwa Wakurugenzi huduma za maji nchini