Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
Imeelezwa kuwa bado Tanzania inakabaliwa na changamoto mbalimbali za majanga ambayo bado yanaongezeka na kuathiri Jamii na kuleta maendeleo hasi.
Aidha majanga hayo yamekuwa yakisababisha maafa na kuleta madhara Kama vile upotevu na uharibifu wa miundombinu,ya umma na binafsi vifo,ukame,ulemavu wa kudumu
Hayo yameelezwa na Meja jenerali Michael Mamunga ambaye ni mkurugenzi wa idara ya menejimenti ya maafa ofisi ya waziri mkuu wakati akifungua mkutano wa wadau wa jukwaa la udhibiti wa majanga Kitaifa,Kwa niaba ya Dkt John Jingu ambaye ni Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu sera,bunge,na uratibu.
Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo Serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu Katika kutekeza Sheria na sera ya maafa itaendelea na kudhibiti maafa Kwa ngazi zote pamoja na kuwa rasimu.
Aliongeza kuwa ili kukabiliana na majanga hayo ambayo yamekuwa yakitokea mara Kwa mara mpango huo pia umeanisha majukumu 14 ambayo yanatakiwa kutekelezwa.
Alitaja majukumu ambayo sasa yanatakiwa kuchukuliwa ambayo ni Huduma za afya,nishati, malazi na utunzaji wa watu,shuguli za ujenzi,usafirishaji,maelekezo ya udhibiti,uzimaji moto,uokoaji,taarifa za dharura za umma,tathimini za uharibifu.
Alihitimisha Kwa kusema kuwa ni wakati muafaka sasa wadau wa jukwaa la maafa lakini hata wale wa sekta binafsi sasa kuungana na kuwa kitu kimoja Katika kuiepusha Jamii dhidi ya majanga yatokanayo na maafa.
Naye Naibu kamisha kutoka Katika jeshi la Zima moto Charo Mangare alisema kuwa wao Kama Zima moto tayari wameshaweka mikakati mbalimbali ya kupambana na majanga ya moto
Alitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kutoa elimu ya nyumba Kwa nyumba ili majanga yatakapotokea waweze kuchukua tahadhari
“Ndani ya mkakati huu ambao tunauisha sasa sisi Zima moto bado tunapata majanga ya kawaida hasa kwenye mioto tunapata lakini tunawapa watanzania elimu ya kabla na baada ya janga kutokea ili linapotokea madhara yasiwe makubwa”aliongeza Mangare
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato