Na MWandishi Wetu, TimesMajira Online, Sabasaba
MAMLAKA ya Uendelezaji Biashara na Masoko Tanzania (TanTrade) imeishukuru Benki ya NBC kwa kuwezesha wajasiriamali kushiriki Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam mwaka huu wa 2020.
Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi wa TanTrade, Latifa Khamis alipotembelea banda la benki hiyo kwenye Viwanja vya Julius Nyerere, maarufu “Sabasaba” ili kutoa shukran kufuatia udhamini huo.
“NBC ni miongoni mwa taasisi ambazo zimekuwa zikituunga mkono kwa miaka minne mfululizo, ni wadau wakubwa wa maonesho haya, kupitia udhamini wao wa shilingi milioni 80 wamewezesha wajasiriamali kushiriki maonesho haya wakiwa na bidhaa zenye viwango vinavyohitajika, bidhaa zao ziko kwenye standards za kimataifa.” Alisema Latifa.
Naye Meneja Uhusiano wa Benki ya NBC William Kalaghe, amewapongeza Tantrade kwa kuwezesha maonesho kufanyika katika kipindi kifupi, na ndio maana NBC iliamua kuwa sehemu ya taasisi zilizounga mkono maonesho haya.
“Sisi ni wadau katika maonesho haya, hatuko hapa tu ili tuonekane bali ni moja ya wachezaji muhimu katika kukuza uchumi wa nchi hivyo tuko hapa kuwaenzi na kuwatunza wajasiriamali ili waweze kutekeleza shughuli zao na tunatoa wito kwao waendelee kushirikiana na TanTrade.” Ameeleza Kalaghe
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi