Na Mwandishi Wetu TimesMajira online,Dar
WAZIRI wa Habari,Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wafanyabiashara ,wajasilimali pamoja na wananchi kujiunga na mfumo wa duka mtandaoni ili kuuza na kununua bidhaa ndani na nje ya nchi.
Dkt.Ndugulile ametoa rai hiyo katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaama katika hafla ya utiaji saini ya makubaliano baina ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE) na Shirika la Posta Tanzania juu ya uendeshaji wa duka la mtandao.
Amesema duka mtandao ni fursa ya kufungua milango ya masoko ya kwa wajasiriamali wadogo wadogo na wakubwa kuuza bidhaa zao ndani na nje ya nchi.
“Kupitia duka mtandao wafanyabiashara watapata fursa ya kuuza bidhaa zao na mtu kupata fursa ya kuipokea popote pale anapokuwa japo hili ni nzuri na kusisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuweka mabadiliko katika shirika la posta kuwa kitovu cha biashara”amesema
Dkt Ndugulile amesema upo umuhimu kuanzisha sheria ya kusimamia taarifa binafsi .
Alisema shirika la posta limefungua zaidi ya vituo 350 na kununua magari 5 lengo kuhakikisha usafirishaji unafanyika kwa haraka na ufanisi.
Aidha aliitaka Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania kuwaamasisha wafanyabiashara kujiunga katika mtandao huu ili waweze kujitagaza na kuuza bidhaa zao.
Vilevile amesma kutokana na Teknolojia kukua kwa kasi ipo haja ya kutangaza maonesho haya kupitia mtandao ambapo mtu atapata fursa ya kuuza na kununua bidhaa popote alipo.
Katika hatua aliliomba shirika la Posta Tanzania kuimarisha mifumo ili watu waweze kununua na kuuza bidhaa zao bila ya kupata chagamoto yoyote.
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo amesema matumizi mengi ya mitandao yamekuwa hayana maslahi katika kukuza uchumi.
” Matumizi yetu ya mtandao zaidi yamejikita zaidi katika mambo ya kawaida yasiyokuwa ya kiuchumi badala ya kitumia katika shughuli za kiuchumi”amesema
Amesisitiza kuwa ni muhimu kutumia miundombinu ya kidijitali kuboresha uchumi ili kifikia malengo ya kimkakati.
Profesa Mkumbo alisema duka mtandao ni fursa nzuri ambayo itamuwezesha mfanyabiashara kufanya biashara bila ya kujenga duka.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi