January 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tantrade, Misri kuaanda mikutano ya b2b

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Latifa Khamis amekutana na Maafisa kutoka Ubalozi wa Misri nchini Ukiongozwa na Mohammad Ally Atteya na Leila Adel, ambapo wamezungumzia maandalizi ya Maonesho na Mikutano ya B2B katika sekta ya Hotel na Vifaa vya nyumbani kutoka Misri.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika tarehe 17-19 Julai, 2023, Zanzibar ambapo Kampuni takriban 15 za Misri kwenye Sekta ya Utalii zitashiriki.

Akizungumza katika kikao hicho juni 20, 2023 katika ofisi za TanTrade Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Latifa Khamis amesema TanTrade itashirikiana na Ubalozi wa Misri katika uratibu kwa kutoa wataalam kutoka TanTrade Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano huo.

Katika Mkutano huo kutakuwa na Maonesho madogo ya Bidhaa pamoja na mikutano baina ya wafanyabiashara (B2B) wa Tanzania Misri.

Pamoja na kuwahakikishia ushirikiano, Mkurugenzi Mkuu aliwakaribisha kutembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 28 Juni -13 July, 2023 katika Uwanja wa Mwl. J. K. Nyerere.