December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tantrade, Iran yaimarisha mahusiano ya biashara na uwekezaji

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Latifa M. Khamis amekutana balozi wa Iran nchini Tanzania, Hussein Alvandi Behineh kujadili ukuzaji wa mahusiano ya kibiashara baina ya Tanzania na Iran Katika Sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu na teknolojia.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika juni 23, 2023 katika Ofisi za Ubalozi wa Iran nchini yenye lengo la kujadili ukuzaji wa mahusiano ya kibiashara baina ya Tanzania na Iran Katika Biashara na Uwekezaji kwa Sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na afya, elimu na teknolojia.

Katika kikao hicho wamejadili kuhusu ushiriki wa Iran kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambapo kutakuwa na siku maalum ya Iran kwa ajili ya kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Iran ili kubadilishana fursa baina yao.

Sambamba na hilo walijadili kuhusu kuratibu misafara ya kisekta zikiwemo afya, elimu na teknolojia mbalimbali.