Na Hadija Bagasha Tanga, Timesmajira Online
MEYA wa jiji la Tanga Abdurahaman Shiloo amesema wamebuni vyanzo vipya vya mapato ikiwa ni pamoja na soko kubwa la kisasa la biashara la jumla katika mji wa Pongwe nje kidogo ya jiji la Tanga.
Shiloo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mara baada ya jiji hilo kushika nafasi ya kwanza kwenye ukusasanyaji wa mapato uliofanywa kwenye majiji sita nchini.
Meya Shiloo Halmashauri hiyo inafikiria kuongeza vyanzo vingine vya mapato ikiwa ni pamoja na kuanzisha soko kubwa na la kisasa litakalokuwa linauza mazao ya jumla ili magari makubwa yanayoleta bidhaa nje ya jiji la Tanga yaishie kata ya Pongwe na yasiingie katikati ya jiji.
“Soko la Pongwe ndio litakuwa linahudumia masoko yetu ya mjini kama Makorora, Nagamiani na sehemu zingine kwahiyo lile sokolikiwepopale litachochea uchumi kwa kuwa soko ni kubwa na eneo pia ni kubwa hivyo ni moja yakitegauchumi kijacho… lakini pia tunategemea kuyaboresha masoko yetu tuliyonayo hivi sasa, “amebainisha Shiloo.
Awali akizungumzia namna halmashauri hiyo ilivyoweza kuibuka kidedea, Meya Shiloo amesema Halmashauri ya Jiji la Tanga imetangazwa kuongoza majiji sita ambayo ni majiji ya Mbeya, Daresalaam, Arusha, Mwanza, Dodoma na Tanga yenyewe ikiwa ndio kinara.
Meya Shiloo amesema wameongoza kwa kukusanya takribani asilimia 56 ya mapato yote ambayo yanatakiwa ambapo mpaka Desemba 31 walitakiwa wawe wamekusanya asilimia 50 lakini wao wameibuka lengo la asilimia hiyo jambo ambalo amesema ni mfano wa kuigwa.
“Nimpongeze Mkurugenzi wa jiji la Tanga na idara yake ya fedha ambayo inahusika na masuala ya makusanyo ya mapato lakini pia niwapongeze watendaji wote wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kwasababu mapato yote hayo yamekusanywa kutoka vyanzo mbalimbali ambapo kila mkuu wa idara na kitengo nao wamechangia kwa namna moja ama nyingine, “alisema Meya Shiloo.
Amesema siri ya mafanikio hayo ni kufanya kazi kwa pamoja kwa kushirikiana na baraza la madiwani, Mbunge, Mkurugenzi, Mkuu wa wilaya lengo likiwa ni kuhakikisha malengo na dira ya taifa ya mwaka 2025 inatimia.
Baadhi ya madiwani wamesema mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano uliopo kati yao na timu ya mkurugenzi wa halmashauri ya jiji.
Katika kipindi cha robo ya kwanza iliyopita, halmashauri ya jiji la Tanga baada ya kushindanishwa na majiji mengine nchini ilishika nafasi ya tatu kwenye ukusanyaji wa mapato.
Meya wa Halmashauri ya jiji la Tanga Abdulrahman Shiloo akizungumza na, waandishi wa habari ofisini kwake namna Halmashauri hiyo ilivyoweza kuibuka katika ukusanyaji wa mapato.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa