Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Mbeya
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) kupitia idara ya masoko, limeendelea na kampeni kabambe ya kuhakikisha inatoa elimu kwa wachimbaji wadogo, kati na wakubwa wa madini pamoja na mashine za kusaga nafaka mkoani mbeya ili wafahamu elimu ya matumizi Bora ya umeme.
Lengo la kampeni hiyo Ni kuhamasisha matumizi bora ya umeme, usalama wa umeme kwa viwanda hivyo, kuunga mkono jitihada za Mh Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha uchumi wa viwanda unafikiwa kwa Kasi nchini na kuongeza Tija kwa Taifa.
Miongoni mwa migodi ambayo imekwishatembelewa mkoani Mbeya ni pamoja na mgodi wa makaa ya Mawe Kiwira, mgodi wa dhahabu Chunya wa Mdimi investment, Mehrab minerals resources, mgodi wa mama Today iliyoko wilayani Chunya.
More Stories
Majaliwa:Serikali imejipanga kukamilisha maandalizi michuano CHAN,AFCON
Uwekezaji ufanyike maporomoko ya maji Kalambo
Bunge lapitisha muswada wa Sheria za kazi,wanaojifungua watoto njiti waongezwa likizo ya uzazi