December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TANESCO yaagizwa kufanya kazi kwa vitendo wananchi wapate umeme

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

NAIBU Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amezitaka taasisi zote zilizo chini ya wizara yake hasa TANESCO kufanya kazi kwa vitendo na kuhakikisha wananchi wanapata umeme kote nchini.

Dkt.Biteko ametoa kauli hiyo wakati akizungumza  kwenye maonesho ya wiki ya Nishati Bungeni jijini Dodoma yaliyolenga kutatua kero za wananchi kupitia wabunge ambao ndio wawakilishi wao.

Alisema wananchi hawataki maneno isipokuwa wanataka vitendo huku akisema vitendo ndivyo vitakavyoleta tija hasa katika upatikanaji wa umeme na hivyo kuleta maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Nataka niwatangazie watanzania kupitia mkutano huu,wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni watu wa kwanza ambao wamekuwa wa kwanza kumerwa na matatizo ya umeme ,tena siyo kwa kusema bungeni tu hadi wanakuja ofidini kwangu kuhakikisha wananchi wao wanapata uneme.” Alisema dkt.Biteko na kuongeza kuwa

“Tunataka kufanya ‘ rebranding ‘ ya TENESCO,na rebranding huwezi kuifanya kwa maneno bali unaifanya kwa kutenda,
lazime tufike mahali TANESCO ibebe taswira nzuri ya kwamba hili ni shirika tegemeo la watanzania 

Alisema,wabunge wamekuwa wakifuatilia suala la umeme kwa karibu kutokana na upatikanaji wa  nishati hiyo hurahisisha hata shughuli za kiuchumi.

“Kwenye vikao vyetu vya chama,wabubge hawa wameshaniweka kitimoto kama mara mbili au mara tatu ,nawapongeza sana waheshimiwa wabunge kwa usimamizi wenu,inawezekana mtu mwingine asione mnachokifanya lakini Mungu ni shagidi kwamba mnafanya kazi kubwa ya kuwasaidia watanzania kupata umeme.”alisisitiza

Aidha amewataka watendaji wa TANESCO kuwa na ushirikiano na wananchi ili kuondoa malalamiko .

Hata hivyo amewapongeza warumishi wa TANESCO kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwapatia umeme wananchi licha ya mazingira magumu hasa katika kioindi hiki cha mvua  wanayokumbana nayo .