December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TANESCO wamuunganishia umeme aliyesaidia kuzalisha Wajawazito wawili nje ya geti la zahanati

Na Ashura Jumapili, TimesMajira Online, Kagera

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO)limemuunganishia umeme Mkunga , Leokadia Samweli,aliyesaidia kuzalisha Wajawazito wawili nje ya geti la zahanati ya Kashai iliyoko manispaa ya Bukoba mkoani Kagera baada ya wauuguzi waliokuwa zamu kugoma kufungua geiti kwa kutumia mfumo mpya wa NI-KONEKT unaowarahisishia wateja kupata huduma kwa haraka zaidi hata akiwa nyumbani kwake kwa kutumia vifaa kama vile simu, kompyuta au kutembelea ‘website’ ya shirika hilo ambayo ni www.tanesco.co.tz.

Akiongea na waandishi wa habari nyumbani kwa Mkunga huyo wakati zoezi la kumfungia umeme likiendelea Ofisa uhusiano na huduma kwa wateja shirika la TENESCO mkoa wa Kagera, Samweli Mandari amesema kuwa wamefanikiwa kumuunganishia umeme kwa maelekezo waliyopewa na Naibu Waziri wa Nishati Wakili Steven Byabato.

“ Tarehe 25 mwezi huu tulipokea maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati Steven Byabato, kwamba sisi kama TANESCO tunatakiwa kushiriki jambo hili kama kutoa mchango kwa jamii ambao ni utaratibu wa kawaida wa shirika kuweza kuchangia masuala ya kijamii, leo tunafurahi tumeweza kumuunganishia umeme bibi huyu ambaye alifanya tukio la kishujaa la kuwasaidia Wajawazito ambao walikuwa wamepata changamoto katika zahanati ya Kashai, na sisi tumemuunganishia umeme bure bila gharama zozote” anasema Mandari.

Amesema shirika hilo limafanikisha huduma hiyo kwa kwa kutumia mfumo mpya wa NI-KONEKT unaowarahisishia wateja kupata huduma kwa haraka zaidi hata akiwa nyumbani kwake kwa kutumia vifaa kama vile simu, kompyuta au kutembelea ‘website’ ya shirika hilo ambayo ni www.tanesco.co.tz.

Naye diwani wa kata ya Kashai iliyoko katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Ramadhan Kambuga amelishukuru shirika la TANESCO , viongozi wa mkoa wa Kagera, wadau mbalimbali pamoja na wananchi ambao wamejitokeza kutoa michango mbalimbali ikiwemo ya vifaa vya ujenzi wa nyumba ya bibi huyo ambayo ujenzi wake umefikia hatua nzuri.

Mkunga huyo Leokadia wakati akiongea na waandishi habari nyumbani kwake baada ya kuunganishiwa huduma ya umeme ,alishukuru uongozi wa mkoa na shirika la umeme la tanesco kumuwezesha hupata huduma muhimu tangu alipowasaidia Wajawazito wawili kujifungua.

“Namshukuru mwenyezi Mungu aliyeniwezesha kufanikisha jambo hilo,naniwashukuru shirika la TENESCO kwa kuniangalia, kuniona na kuniinua na mimi nisifadhaike tena maana nilikuwa natumia kibatari ila pia namshukuru diwani pamoja na mbunge wa jimbo la Bukoba mjini aliyeagiza kutekeleza jambo hili leo nimeunganishiwa umeme”anasema Mkunga huyo.

Tukio hilo la kishujaa lililofanywa na Mkunga Leokadia Samweli la kuzalisha Wajawazito wawili nje ya geti ya zahati ya Kashai lililotokea Julai Mosi mwaka huu majila ya saa 10 alfajiri baada ya wauguzi waliokuwepo zamu kugoma kufungua geti la Zahanati hiyo na kuwahudumia Wajawazito.


Wa kwanza kushoto diwani kata Kashai Ramadhan Kambuga,akifuatiwa na Mkunga Leokadia Samwel na aliyevalia kofia ngumu ni Ofisa uhusiano tanesco mkoa wa Kagera Samwel Mandari.
Fundi wa tanesco akiunganisha umeme nyumba ya Mkunga iliyojengwa na wadau mbalimbali.
Ofisa uhusiano tanesco mkoa wa Kagera Samwel Mandari akimkabidhi Mkunga rimoti ya kuwekea umeme