November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tamgo yazinduliwa, yaja na teknolojia ya kutibu maji chumvi kwa matumizi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kampuni Tamgo ambayo inajishughulisha na utengenezaji wa mitambo ya kutibu maji, umeme wa nishati ya jua (solar system) na magenerata imezinduliwa rasmi nchini.

Uzinduzi huo ulifanyika jijini hivi karibuni kwa lengo la kutoa huduma bora za vifaa hivyo vya kisasa hapa nchini vyenye ubora wa hali ya juu.

Meneja uendeshaji Henrik Nielsen alisema kuwa wamejipnga katika soko la ushindani la hapa nchini, lakini vifaa bora ndiyo nguzo yao kubwa ya kushinda soko.

Alisema kuwa waajivunia uzoefu katika sekta ya utengenezaji mitambo ya kisasa ambapo wamefanya hivyo katika nchi nyingi na kuamua kupanua biashara yao hapa nchini.

“Tunajua kuna ushindani mkubwa katika soko, lakini nguzo yetu kubwa ni kutoa huduma bora na za kisasa zaidi kama tulivyofanya katika nchi nying ambazo tumekuwa na biashara ya aina hii,” alisema Nielsen.

Kwa upande wake, Meneja wa kampuni hiyo, Tarek Mostafa alisema kuwa wanajivunia uwekezaji mkubwa wa teknolojia ya tiba za maji, genereta na umeme wa nishati ya jua katika maeneo yote wanayofanya biashara duniani.

Wakati huo huo, Mkuu wa idara ya maji wa kampuni hiyo, Damian Massenge alisema kuwa wametengeneza mtambo wa kuchakata maji ya chumvi ujulikanyo kwa jina Reverse osmosis (RO) na kuwa maji matamu.

Massenge alisema kuwa alisema teknolojia hiyo inapatikana kote nchini kwa muda mfupi na gharama nafuu akifafanua kwamba itasaidia kuondoa chumvi kwenye maji katika maeneo ambayo yana maji chumvi.

Alisema kuwa wamejifunza kutoka kwenye nchi za Ujerumani, Italia na Ufaransa.Alifafanua kwamba upatikanaji wa maji ya chumvi ni rahisi hasa kipindi hiki cha ukame, hivyo wanapoyachakata na kuondoa chumvi itapunguza makali ya mgao kipindi hiki.

“Mitambo hiyo ya kisasa inazalishwa hapa hapa nchini na kuwarahisisha upatikanaji wake na hivyo kupunguza gharama tofauti na miaka ya nyuma ilikuwa lazima ikatengenezwe nje ya nchi na kuanza kuisafirisha ambapo gharama iliongezeka zaidi,” alisema.

Meneja uendeshaji wa kampuni ya Tamgo Tanzania Henrik Nielsen akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo hapa nchini.
Meneja uendeshaji wa kampuni ya Tamgo Tanzania Henrik Nielsen (Katikati) akizungumza na maofisa wengine wa kampuni hiyo wakati wa uzinduzi rasmi hapa nchini.
Wafanyakazi wa kampuni ya Tamgo Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi rasmi hapa Tanzania.