Na Sarah Kassim, TimesMajira Online
Wakala wa ufundi na umeme Tanzania (TEMESA)waboresha matumizi ya kadi ili kuepusha msongamo wa foleni wa kujaza kadi
Akizungumza na Gazeti la Majira, leo Oktoba 19,2022, Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano ya umma Alfred (Oktobar 19, 2022) amesema kuwa maboresho hayo ni kwa upande wa NITC, kujaza kadi kwa kulipia kwa njia ya mitandao ya simu kwa watumiaji.
Aidha Alfred amesema wamekua wakitoa elimu mala kwa mala kwa watumiaji wa kadi hizo kwani wengi wamekuwa wakishindwa kujua namna ya matumizi na faida zake kwa ujumla.
“Tumetoa Elimu ya matumizi ya kazi na matangazo kwa pantoni tumebolesha kwa kulipia kwa mitandao ya simu kwa kupunguza msongamano wa kujaza kadi.”amesema Alfred
Pia amesema kumekuwa na tatizo la Kugoma kwa kadi ambapo tatizo hilo ni suala la mtandao kusumbua au mtandao wa simu aliotumia mteja kujaza kadi.
Hata hivyo meneja vivuko kanda ya Mashariki na Kusuni, Lokombe King’ombe amesema kuwa Elimu ya kadi inaendelea kutolewa katika vivuko vyote ili mtumiaji aweze kujua kwa wepesi matumizi ya kadi hiyo na elimu hiyo itakuwa ni endelevu.
“Elimu ya matumizi ya kadi inatolewa kila kivuko na maswala ya Kugoma kwa mashine ni maaswala ya mtandao sio temara.”amesema lokombe
Kwa upande wake Mfanyabiashara kutoka Ferry, Rahma Hamisi ambaye ni mtumiaji wa kadi alisema elimu ya matumizi ya kadi na jinsi ya kulipia kwa mtandao ya simu inasaidi kuwaondolea msongamano wa foleni wakati wa kupata huduma.
“Elimu ya matumizi kadi na jinsi kulipia kwa mtandaoya simu inatusaidia kuondoa file.”
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti