UTAFITI wa hivi karibuni unaonesha kuwa wastaafu wanaweza kuingiza kiasi kikubwa cha fedha katika kuelekea uchumi wa viwanda kutokana na mafao wanayolipwa, ambapo kama wastaafu watawekewa mfumo mzuri wanaweza kujiinua kiuchumi.
Ingawa kwa upande mwingine utafiti unaonesha ya kuwa wastaafu wengi hawana fursa ya kupewa mikopo kutokana na taasisi za fedha kuwa na hofu ya usalama wa mikopo yenyewe, kwa imani kuwa wastaafu ni wazee, hawana umri mrefu wa kuendelea kuishi tena au wakati mwingine kwa wastaafu wenyewe kutokuwa na elimu ya kuendesha miradi inayoweza kuwapatia faida na kurejesha mikopo hiyo.
Hapa ijulikane ya kuwa wastaafu ni watumishi wenye uzoefu na mchango mkubwa katika nyanja mbalimbali na kustaafu kwao kunatokana na masharti ya ajira. Ingawa ikitokea upunguzwaji wa wafanyakazi sehemu za kazi mtu wa kwanza anayefikiriwa kupunguzwa anakuwa ni mstaafu mtarajiwa.
Ingawa fedha za malipo za pensheni hazitoshelezi kukidhi mahitaji yao ya lazima kimaisha kama kusomesha watoto, gharama za matibabu na kuanzisha miradi ya kujiendeleza. Na matokeo yake wastaafu wengi wameishi kwa kuunga unga tu bila ya kuwa na vyanzo vya fedha vyenye uhakika.
Ili kupambana na hii hali, hivyo basi kuna haja kubwa ya kuwepo kwa mafunzo maalumu kwa wafanyakazi wanaokaribia kustaafu ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na maisha mara baada ya kustaafu kulitumikia taifa.
Miongoni mwa mambo muhimu ambayo wastaafu wanatakiwa kufundishwa ni kama vile kuwaaanzishia viwanda vidogo vidogo, kuweka akiba, jinsi ya kuwekeza na namna bora ya utunzaji fedha kwenye taasisi za fedha, na mbinu mbalimbali za ujasiriamali.
Pamoja na hayo wafanyakazi wanaotarajia kustaafu wanatakiwa pia kuandaliwa kwa kukumbushwa juu ya kuzingatia mabadiliko ya maisha kutoka katika utumishi wa umma kwenda katika mfumo wa maisha ya kawaida na kuwahamasisha kuanza kutambua vipaji vyao vya ujasiriamali bado wangali kazini ili kujiepusha kufanya miradi ambayo hawana ujuzi wa kutosha baada ya kustaafu.
Mifuko ya hifadhi ya jamii pia inajukumu kubwa la kuhakikisha ya inawajengea uwezo wanachama wao wakati bado wangali kazini ili wawe na mbinu za kuendana na mazingira hayo mara tu ya kustaafu kwao, hivyo ni jukumu na wajibu wa mifuko kutambua umuhimu wa wastaafu na faida za kujiandaa kustaafu.
Hivyo ni jukumu la mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kusaidiana na waajiri kuwaandaa wanachama kabla ya kustaafu juu ya stadi mbalimbali za kuongeza kipato, ikiwemo na jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza baada ya kustaafu na jinsi ya kuishi mtindo wa maisha bora baada ya kustaafu.
Hapa ikumbukwe ya kuwa jukumu la kutambua ya kuwa kuna siku ya kustaafu katika maisha ya binadamu ni suala la kila mtu. Kwa sababu kama binadamu mfanyakazi lazima utambue ya kuwa ni muhimu kujiandaa vyema na maisha mapya ya baada ya kustaafu ambayo kimsingi yatakuwa tofauti na haya ya wakati huu unapofanya kazi kama mwajiriwa.
Hivyo kila mfanyakazi lazima atambue ya kuwa kuwa ni mstaafu mtarajiwa hivyo kujiandaa kwake ni jambo muhimu na anahitajika kuanza kubadilika kifikra katika maisha yake ya kila siku.
Na ikumbukwe ya kuwa kadiri tunavyo kuwa wazee tunafanya kazi, tunazalisha na kipato chetu kinazidi kuwa kidogo zaidi na hivyo basi tunahitaji kupata kipato kutoka sehemu nyingine ili kuhakikisha ya kuwa tunaendeleza maisha yetu.
Lakini mipango hii inatugusa sisi wote kwani haijalishi kwa sasa wewe in tajiri au maskini, halijalishi wewe ni mtoto au mtu mzima au una umri wa miaka mingapi kwa sasa mipango hii iiliyoiridhiwa inaweza kusaidia malengo hayo au ikawa ndiyo kizuizi cha kukua kwa maendeleo ya uchumi na kijamii nchini.
Ikumbukwe ya kuwa idadi ya Watanzania wanaofikia umri wa uzee unazidi kuongozeka kila siku, kinga ya hifadhi ya jamii ya wazee nayo inazidi kuingia kwenye matatizo zaidi. Kwa sababu sekta isiyo rasmi ya kijamii na mfumo wa hifadhi ya jamii unaotolewa na familia unazidi kupungua na kuwa dhaifu siku hadi siku.
Na mfumo wa hifadhi ya jamii ulio rasmi kama vile unaotolewa na taasisi hizi zetu za hifadhi ya jamii za kuchangia na zile zisizo za kuchangia zinakabiliwa na utumiaji ovyo wa michango ya wanachama kwa kuwekeza kwa kufuata maangizo ya wanasiasa.
Na kwa upande mwingine bila kutumia vitego vya kitaalamu na kuwa na matumizi makubwa ya michango ya pensheni za wanachama bila vile vile bila ya kufuata kanuni na utaratibu wa uwekezaji michango ya wanachama.
Kwa ujumla ni kwamba mifuko haina utaratibu wa kufuata utawala bora wa jinsi ya kuendesha taasisi hizi za hifadhi ya jamii, na matokeo yake idadi kubwa ya wazee ambao wamekuwa wakichangia katika kujenga taifa hili kwa muda mrefu hawana hata kinga ya uzee yaani kupatiwa mafao ya kustaafu ya kutosheleza mahitaji muhimu ya maisha yao ya kila siku.
Mpaka sasa hakuna mfuko hata mmoja wa hifadhi ya jamii unaodhubutu kutoa maelezo halisi ya mwenendo wa hifadhi ya jamii nchini. Leo ukidadisi juu ya idadi ya wazee wanaopata pensheni kila mwezi ni idadi ndogo sana ukilinganisha na idadi ya wazee wanaostaafu kila siku.
Hii ina maana mifuko haiko karibu na wastaafu wao, huenda unaweza ukakuta hawana hata kumbukumbu sahihi za wastaafu wao zinazoonesha vitongoji au vijiji vyao, wilaya na hata mikoa yao pamoja na kuwa na ofisi za mifuko hii ziko karibu mikoa yote ya Tanzania. Mtu mwingine na wakati mwingine anaweza akakwambia huenda labda ni kwa sababu ya ukosefu wa elimu ya hifadhi ya jamii miongoni mwa wastaafu.
More Stories
Ubunifu wa Rais Samia kupitia Royal Tour unavyozindi kunufaisha Tanzania
Rais Samia anavyojenga taasisi imara za haki jinai kukabilina na rushwa nchini
Rais Dk. Samia alivyowezesha Tanzania kuwa kinara usambazaji umeme Afrika