November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Pamela Kikuli

Tamasha Safari Nyoma Choma kufanyika Novemba 29

Na Angela Mazula, TimesMajira Online.

MASHINDANO ya Tamasha la Safari Nyama Choma ambalo likizijumuisha Bar takribani 60 huku 10 ndizo zitaingia fainali, linatarajiwa kufanyika Jumapili ya Novemba 29 mwaka huu, katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jjijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Safari Lager Pamela Kikuli amesema, lengo ni kutaka kuwakutanisha pamoja wapishi wazuri wa nyama choma na kuwashindanisha ili kuongeza ubora wa kazi wanazozifanya kila siku.

‘’Tumewatumia walimu wa mapishi kutoka Tanzania Bara na Visiwani, kama majaji wa shindano hili, ambapo mpaka sasa zimebaki siku mbili kutimiza idadi ya washiriki wote ambao watakuwa wamefanikiwa kuingia fainali za mashindano hayo yatakayofanyika Kijitonyama katika viwanja vya Posta, amesema Kikuli.

Amesema, kwa kutembelea bar mbalimbali na kuangalia namna ambayo wanaandaa chakula hicho kwa kuanzia na maandalizi, hali ya usafi kiujumla ni moja ya sifa ambazo majaji walikuwa wanaangalia.

Hata hivyo amesema, aina ya nyama pia huongeza ubora mara baada ya nyama hizo kuchomwa na mpaka sasa tayari baa 8, zimepata nafasi ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha fainali kwani tunatarajia kushirikisha baa 10 ambazo zitaingia fainali.

‘’Zipo zawadi nyingi katika shindano hilo la Safari Nyama Choma, fedha taslimu sh. milioni 2, kupewa cheti cha ushiriki, sare za chief ambazo zipo zinazotambulika na kuonyesha ubora wa kazi zao, amesema.

Kwa bar ambayo itapata nafasi ya ushindi pia itapa nafasi ya kujitangaza zaidi na Tamasha hili la ‘Safari Nyama Choma’ ambalo hufanyika hapa nchini na kuandaliwa na bia ya Safari Lager.

Naye Jaji Mkuu wa shindano hilo Fredy Uwiso amesema ‘’sio tuu kuwapata washindi wazuri wa nyama choma kutoka kwenye bar mbalimbali hapa nchini bali hata kuonyesha uwezo wa wapishi wazuri waliopo kimataifa kwa kushiriki shindano hilo’’.

Amesema Uwekezaji mzuri kwenye majiko ya bar ni jambo la msingi kwani biashara yeyote inahitaji uwekezaji mkubwa na mafanikio yake pia huwa mkubwa kwani mafanikio yeyote huenda sambamba na uwekezaji wa muda na fedha.

Akitolea mfano kuwa mpishi wa bar huonekana bora kuanzia kwenye mavazi yake kuwa masafi na pia humvuta mteja kwani watu hupenda kula wanachokiona na sio kusimuliwa.

Amesisitiza kuhusu watalii ambao wanakuja hapa nchini kuweza kutembelea bar mbalimbali zikiwa na kiwango chenye ubora unaostahili kitu ambacho kitaongeza pato la bar hizo.