December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tamasha la harusi kufanyika Julai 16

Na Yusuph Digossi, Timesmajira Online

TAMASHA la maonesho ya mavazi ya harusi lijulikanalo ‘Adorable Weadding Trade Fair’ linatarajiwa kufanyika Julai 16 mpaka 18 mwaka huu, kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

Akizungumza na gazeti hili muandaaji wa tamasha hilo Anna Lema, amesema tayari maandalizi yamekamilika hivyo ameomba wadau na maharusi watarajiwa kujitokeza kwa wingi ili kutimiza ndoto zao.

“Mwaka huu tunavitu vingi vipya tofauti, hasa tunawakaribisha maharusi kufika ili kupata nguo za kisasa zinazoenda na wakati pia kukutana na watoa huduma mbalimbali wakiwemo washereheshaji,”amesema Anna Lema.

Anna Lema amesema, kutakuwa na droo itakayochezeshwa kwa maharusi watarajiwa na washindi watapata nafasi ya kufanyiwa harusi bure na watoa huduma hao kama ilivyo kuwa hapo awali.

Aidha amesema, mwaka huu wanatarajia kuwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo, ambaye atahudhuria na kuongea na watoa huduma pamoja na wadau mbalimbali ili kuboresha sekta hiyo.