September 15, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TALGWU kufanya Mkutano Mkuu kupitia taarifa ya maendeleo

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online,Dodoma

CHAMA cha wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kinatarajia kufanya Mkutano mkuu wa Taifa kwa kuzingatia ibara ya 55.1 ya katiba ya chama ya toleo la mwaka 2026.

Akitoa taarifa ya Mkutano huo Mkuu wa kitengo na Mawasiliano wa chama na Mratibu wa uchaguzi 2026 Shani Kibwasali,amesema Mkutano huo utafanyika tarehe 17 na 18 Septemba mwaka huu katika ukumbi wa Mkutano wa St.Gasper Jijini Dodoma.

Akitoa ufafanizi wa Mkutano huo amesema kuwa Mgeni rasm anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi,Ajira na Mahusiano,Deus Sangu.

Amesema Mkutano huo utafuatiwa na baraza kuu Taifa tarehe 19 Septemba mwaka huu.

Amesema pamoja na mambo mengine,Mkutano mkuu utapitia taarifa ya kazi ya miaka mitano,Kwa maana ya mwaka 2021 na 2026.

Aidha amesema kuwa kutafanyika uchaguzi wa kuwachahua viongozi wa kukiongoza chama kwa kipindi cha mwaka 2026 na 2031 ambapo kwa sasa Mwenyekiti wa chama hicho ni Tumaini Nyamhokya

Katika hatua nyingine ametoa hamasa kwa wanachama wote kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika chama hicho.