Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inawauchunguza wabunge wa Chadema kuhusu matumizi ya fedha ndani ya chama hicho kwani yanaweza kupatikana makosa ya ubadhirifu na ufujaji wa fefha za chama na matumizi mabaya ya mamlaka.
Taarifa ya Takukuru kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Doreen Kapwani imesema kuwa makosa hayo yote yanaangukia katika sheria ya Takukuru Naomba 11 ya mwaka 2007 inayoongoza chombo hicho.
“Mpaka sasa tayari tumeshafanya mahojiano na viongozi wa Chadema, viongozi waliowahi kuwa Chadema, wabunge waliotoa taarifa na maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,” imeeleza taarifa hiyo
Imeendelea taarifa hiyo ” Pia tumefanya mahojiano na viongozi wa bodi ya wadhamini wa Chadema na sasa tunawahoji wabunge wanachama wa Chadema na wabunge waliowahi kuwa wanachama wa Chadema.”imesema sehemu ya taarifa huyo.”
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja