Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), imeanza kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, inazokikabili Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Brigedia Jenerali John Mbungo, amenukuliwa jana na mtandao mmoja wa kijamii akisema; “Kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo kuna matumizi mabaya ya fedha za michango ya wanachama, wanayochanga kwa mujibu wa Katiba yao”
Watakaohojiwa kuhusiana na sakata hilo ni aliyekuwa Katibu Mkuu CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji (ambaye sasa amehamia CCM) Mkurugenzi wa Itifaki na Mambo ya Nje, John Mrema na Mhasibu wa chama hicho Dkt. Roderick Lutembeka,
Aidha, Mkurugenzi huyo alisema wameshindwa kumhoji Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwa kuwa aliieleza TAKUKURU kwamba yuko nje ya jiji la Dar es Salaam.
Alisema TAKUKURU ilishaanza kukusanya nyaraka kutoka sehemu mbalimbali na kwamba imekuwa ikipata ushirikiano mzuri kwenye suala hilo
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam