Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MKUU wa Mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila ,ameagiza TAASISI ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)wilaya ya Temeke kuwamata viongozi wanaodaiwa kula pesa za miradi ya shule Sekondari Lumo wilayani Temeke.
Mkuu wa mkoa Albert Chalamila alisema hayo wakati wa mkutano wa hadhara Jimbo la Temeke uliofanyika Viwanja vya Lumo baada kumaliza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kutatua kero mbali mbali za wananchi.
“Ninaagiza TAKUKURU Temeke na OCD wa Temeke kuwamata walioiba vifaa vya shule katika shule ya sekondari Lumo wanaodaiwa wote wakibainika na hatia waende Mahakamani sheria ifuate mkondo wake maendeleo yoyote hayana chama awe wa Chama cha Mapinduzi CCM au Chama cha Maendeleo CHADEMA wakamatwe sheria iweze kufanya kazi yake” alisema Chalamila.
Mkuu wa mkoa Chalamila alisema mali ya umma katika miradi ya Rais Samia suluhu Hassan kila mmoja aone maji ya Betri hayafai kunywa na katika mkoa wangu sitaki usanii waliohujumu majina yake tunayo wakamatwe mara moja .
Katika hatua nyingine alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa katika nchi hii atutaki Taifa letu la Tanzania liingie katika machafuko ,Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA waliomba kufanya maandamano walipewa kibari Demokrasia ilifuata maandamano hayakuwa na fujo ila inakuwaga ukolofi wa watu Fulani sasa hivi tunawaruhusu tena CHADEMA wakiomba kibari.
Aliwataka chama cha Mapinduzi CCM kuandaa hoja za msingi ili waweze kuzileta watu waje upande wa pili .
Mkuu wa shule ya sekondari Lumo Frida Kyando alisema taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 32 vya madarasa ya ghorofa shule ilianzishwa April 2007 kwa sasa ina walimu 31 wanawake 22 wanaume 9 jumla ya wanafunzi 1706 wanawake 837 wanaume 869.
Aidha alisema mradi huo wa shule ya sekondari ya gorofa una vyumba 32 vya madarasa ,ofisi za walimu 16 matundu ya vyoo 96 utekelezaji wa mradi umeanza wa awamu ya kwanza January 2023 na awamu ya pili February 2024.gharama za mradi wote shilingi bilioni 2.4 fedha iliyopokelewa shilingi bilioni 1.6.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi