Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kuwa hakuna viashiria vya rushwa kwenye mchakato wa zabuni wa kuwapata wakandarasi wa ujenzi wa miradi mkoani Mbeya huku ikionya kuwa inafuatili kwa ukaribu miradi hiyo ili isihujumiwe.
Ambapo Serikali ipo kutekeleza miradi mbalimbali mkoani Mbeya ikiwemo ya ujenzi wa njia nne ambao utaanzia Kata ya Nsalaga hadi uwanja wa ndege wa Songwe, utakaogharimu bilioni 138.7.
Huku ujenzi wa mradi wa maji wa Kiwira wenye thamani ya bilioni 117.5,miradi ambayo ni mikubwa kutekelezwa jijini Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya leo Machi 24,2023,Kaimu Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mbeya, Vangsada Mkalimoto amesema wameanza kufuatilia mchakato wote wa utekelezaji wa miradi hiyo tangu ilipoanza lakini hawajabaini uwepo wa viashiria vya rushwa.
Amesema Takukuru inaendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo na mengine ili kuhakikisha kuwa haifanyiwi hujuma na fedha za serikali zinatumika ipasavyo kama zilizvyoanishwa kwenye mkataba na mpango kazi wa miradi hiyo.
Akizungumzia utendaji kazi wa miezi mitatu wa Takukuru amesema upande wa Jamhuri umeshinda jumla ya mashauri tisa kati ya kumi yaliyofunguliwa na kuamriwa kwenye mahakama mbalimbali za Mkoa wa Mbeya.
“Katika eneo la mashtaka, Takukuru Mkoa wa Mbeya iliendesha jumla ya mashauri 17 katika mahakama mbalimbali za Mkoa , kupitia mashauri haya, mashauri 12 ni yale yaliyokuwa yakiendelea mahakamani hadi kufikia Septemba 31, mwaka jana na mashauri matano ni mapya yaliyofunguliwa katika kipindi hiki na jamhuri ilishinda mashauri tisa,”amesema.
Mkazi wa Uyole Jijini Mbeya ,Rehema Juma amesema kuwa ufutiliaji wa miradi unaofanywa na serikali umekuwa ni faraja kubwa kwa wananchi.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato