Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU (PCCB) Mkoa wa Mbeya imewaunganisha  wananchi zaidi ya 1,624 kwa ajili ya ufuatiliaji wa miradi  ya maendeleo lengo  likiwa ni kuongeza wigo wa mapambano dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za serikali katika miradi pamoja na vitendo vya Rushwa miongoni mwa watendaji wa Serikali .
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya ,Abdaudi Mbura amesema hayo leo ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya robo mwaka ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa waandishi wa habari.
Mbura amesema kuwa wamefanya hivyo wakiamini kwamba vijana na wananchi wakielimika wataweza kuibua taarifa za vitendo vya rushwa katika jamii ikiwemo taarifa zitakazohusu utekelezaji wa miradi inayojengwa chini ya kiwango.
“Kupitia kundi hili ambalo tumetoa mafunzo tutaweza kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuisaidia serikali katika kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inakuwa na ubora unaotakiwa “amesema.
Aidha Naibu Mkuu wa TAKUKURU huyo amesema pia TAKUKURU  imefanya ukaguzi wa miradi 44 ya Maendeleo yenye thamani ya Sh 7.386 Milioni ikiwepo ,Maji,elimu ,barabara na ujenzi wa vyumba vya madarasa kupitia fedha za uviko 19.
Mbura amesema kuwa kwa kipindi hicho pia wamefanya ufuatiliaji kwa watendaji wa kata kwa kata vijiji kwa vijiji mkoa wa Mbeya kufuatilia utekelezaji wa miradi ya Maendeleo pamoja na kuwashirikisha Wananchi namna ya ufuatiliaji wa miradi ya inayoelekezwa na Serikali katika maeneo yao.
Amesema kwa kushirikisha katika na jamii katika kupambana na matukio ya rushwa wameweza kupokea taarifa 109 kati ya hizo 40 hazihusiani na matukio ya rushwa huku kesi mpya zikiwa sita na kesi 25 bado zinaendelea kusikiliza mahakamani na kesi moja Takukuru ikiwa imeshinda.
Aidha amefafanua kwamba katika kufanikisha mapambano dhidi ya vitendo hivyo wameweza kuwafikia Wananchi 2,913 kuwapatia elimu kupitia Mkutano wa hadhara, vilabu vya wapinga rushwa,michezo na mfumo wa upokeaji taarifa wa TAKUKURU inayotembea.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu