Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
TAASISI ya Kizuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Dodoma imeanza kufuatilia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara na mradi usafi wa Mazingira vijijini yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni 10 ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha inapatikana.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma kuhusu taarifa ya taasisi hiyo kwa kipindi cha Julai hadi Septemba ,Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Sostenes Kibwengo amesema ,ufuatiliaji huo unafanywa kwa kushirikiana na wakala wa Barabara za vijijini (TARURA) na Wakala wa Maji safi na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) mkoa wa Dodoma .
“Agost mwaka huu TARURA mkoa wa Dodoma ilisaini mikataba 43 na wakandarasi mbalimbali kwa kazi ya ujenzi wa barabara katika wilaya zote za mkoa wa Dodoma zenye thamani ya jumla ya sh.10.213 milioni inayotekelezwa awamu ya kwanza kwa mwaka 2021/2022 ,
Ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi katika maeneo yanayotekelezwa miradi hiyo kuwa makini kuifutilia kwani ushirikiano wao ni silaha muhimu ya kufikia lengo la miradi hiyo huku akiwataka wakandarasi na wasimamizi wa miradi hiyo kutimiza wajibu wao kwa weledi na uaminifu.
Vile vile amesema pia taasisi hiyo imekagua miradi mingine 17 kwenye sekta za Elimu ,afya na kilimo kwa lengo la kuhakikisha fedha za umma zinazoelekezwa kwenye miradi hiyo zinatumika kwa ufanisi na uaminifu ambapo ufuatiliaji huo umewezesha kuoakoa na kudhibiti fedha na vifaa vyenye jumla ya sh.47.827 milioni ambapo kati yake ni vifaa vyenye thamani ya shilingi 41.950 milioni vilivyochepushwa kutoka kwenye mradi wa ujenzi wa hospitali mojawapo mkoani humo.
Aidha Kibwengo amesema katika robo ya Oktoba hadi Disemba mwaka huu TAKUKURU mkoa wa Dodoma ,imeweka msisitizo katika kuwashirikisha vijana kupitia ushirika wa utatu wa TAKUKURU ,Chama cha Skauti Tanzania na Idara ya Walimu .
“Vijana wa skauti wataelimishwa kuhusu mbinu na umuhimu wa kushiriki katika kuzuia rushwa ili nao wafikishe elimu hiyo kwa vijana wenzao,nyumbani na kwenye jamii kwa ujumla.” Amesema Kibwengo
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito