Na Mwandishiwetu,Timesmajira
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Kinondoni (TAKUKURU) imeunda tume itakayochunguza miradi miwili ya maendeleo kwenye sekta ya afya Manispaa za Ubungo na Kinondoni baada ya kubaini mapungufu kwenye miradi hiyo
Akitoa taarifa ya miezi mitatu ya kipindi cha kuanzia April hadi Juni mwaka 2025 kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mkuu wa TAKUKURU Kinondoni Christian Nyakizee amesema katika kipindi hicho walitekeleza majukumu mbalimbali ikiwepo kufuatilia miradi ya maendeleo, kuendesha programu rafiki, kutoa elimu kwa umma na kufanya uchunguzi wa tuhuma mbalimbali
” Kama mnavyofahamu katika jitihada za kuzuia vitendo vya rushwa TAKUKURU ina jukumu la kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha inatekelezwa kwa ufanisi lakini pia thamani ya fedha katika miradi hiyo ” amesema Nyakizee
Amesema katika kutekeleza jukumu hilo TAKUKURU ilifuatilia utekelezaji wa miradi minne ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni moja na kati ya miradi hiyo miradi miwili katika Sekta ya Afya ilibainika kuwa na mapungufu
Nyakizee amesema mradi wa ujenzi wa jengo la magonjwa ya mlipuko katika Zahanati ya Kijitonyama wenye thamani ya sh. milioni 150 ulikutwa na mapungufu kwenye gharama za ujenzi wa jengo hilo
Amesema pia TAKUKURU ilibaini mradi wa ujenzi wa jengo la upasuaji na wodi ya wazazi katika Zahanati ya Mpigi Magohe Manispaa ya Ubungo ulikutwa na mapungugu kwenye madirisha na kusababisha uharibifu wakati wa msimu wa mvua
“TAKUKURU baada ya kubaini mapungufu hayo tumechukua hatua na kuanzisha uchunguzi ili kuthibitisha thamani ya fedha kwenye miradi hiyo, kuitisha kikao na wadau ambao ni halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ili kukubaliana kufanya marekebisho kwenye mapungufu yaliyobainika ” amesema Nyakizee
Amezitaja kazi zingine ambazo zimefanywa kwenye kipindi hicho kuwa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma kupitia semina, mikutano ya hadhara ,maonyesho na vipindi vya redio
Amesema elimu hiyo imeweza kuleta ufanisi wa usimamizi wa miradi ya maendeleo, pia wananchi wameweza kuhamasika kutoa taarifa za vitendo vya rushwa katika ngazi ya mitaa, vijiji na kata
Ameongeza kuwa utekekezaji wa programs ya TAKUKURU rafiki uliendelea kwa kufanya vikao katika kata 12 ambapo kero 40 ziliibuliwa na kutatuliwa kupitia vikao vya mrejesho
” Kupitia programu hii tulifanikiwa kurejesha viti kumi vya kulalia wagonjwa kutoka ofisi ya Kata ya Tandale vilivyokuwa havijulikani vilipoenda, na kwanba moaka sasa tayari vimerejeshwa na kukabidhiwa kwa viongozi wa kata hiyo ” amesema Nyakizee
Amesema kuhusu uchunguzi na mashitaka malalamiko 120 yalipokelewa katika kipindi hicho ambapo 76 yalihusu vitendo vya rushwa na 44 mengine yako kwenye hatua mbalimbali

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi